Wakati dunia ikizidi kuelekea kwenye matumizi ya smartphone zaidi, kampuni zinazo tengeneza programu mbalimbali za kompyuta nazo pia ziko kwenye harakati za kuhakikisha zinaendana na kasi hiyo ili kuhakikisha hazipotezi wateja kutokana na mabadiliko hayo.
Moja ya kampuni ambayo inaonekana kufanya hivi kwa sasa ni kampuni ya Microsoft. Microsoft imeonekana kuangazia zaidi kwenye ulimwengu wa smartphone huku ikitengeneza nyezo na programu mbalimbali za kusaidia kunganisha wateja wake wa programu za kompyuta kupitia simu za mkononi maarufu kama Smartphone.
Moja ya programu ambayo imezinduliwa hivi karibuni ni programu ya All-in-one Microsoft Office, programu hii inasaidia sana hasa kwa wale ambao wanapendelea kuangalia na kuandika document mbalimbali kupitia simu za mkononi. Kama zilivyo programu za Microsoft Office au Exel ambazo nazo zipo kwenye masoko mbalimbali ya programu za simu, app hii mpya ya All-in-one Microsoft Office imelenga kurahisisha zaidi matumizi ya programu hizo maarufu kwa ajili ya ofisi.
All-in-one Microsoft Office hii ni programu ambayo inajumuisha programu zote za Office za Microsoft ambazo zinapatikana Play Store, yaani kuliko kuwa na programu nyingi kwenye simu yako yaani Word, Excel, PDF na PowerPoint sasa unahitaji app moja tu ya All-in-one Microsoft Office na utakuwa na uwezo wa kuwa na programu hizo zote kwenye app moja tu.
Mbali ya kuwa app hii inajumuisha app zote ndani ya app moja, pia inakuja na sehemu mpya mbalimbali ambazo zinaweza kusaidia sana kurahisha matumizi yako ya kiofisi. Kwa mfano unaweza kupata sehemu ya kusoma QR Code ikiwa pamoja na sehemu ambayo unaweza kutumia kuweka sahihi kwenye documenti mbalimbali za PDF.
App ya All-in-one Microsoft Office pia inakuja na uwezo wa kusaidia kuhifadhi mafaili yako mtandaoni na pia njia mpya ya kushiriki mafaili au document na watu mbalimbali walio karibu pamoja na sehemu mpya ambayo inaweza kukusaidia kubadilisha jedwali lililopo kwenye picha na kuliweka kwenye mfumo wa jedwali la Exel, pamoja na mambo mengine mengi.
Kwa sasa programu hii inapatikana kwenye masoko yote ya Android na iOS na unaweza kupakua app hii kwenye simu yako kupitia link hapo chini.