Hapo siku ya jana kulizuka habari mpya juu ya alama ⚫ yenye uwezo wa kuharibu au (kucrash) programu ya WhatsApp. Ripoti zinasema kuwa kuharibikwa kwa programu ya WhatsApp kunatokea pale mtu unapo kutumiwa meseji ya WhatsApp yenye alama hii <⚫> na endapo ikitokea umebofya alama hiyo ndani ya meseji uliyo tumiwa, basi programu yako ya WhatsApp itakwama na (kucrash).
Kwa mujibu wa ripoti mbalimbali, meseji hiyo inakuja na alama kadhaa ambazo hazionekani ambazo zimeongezewa katikati ya alama ya <⚫> ambazo ndio zinaweza kuharibu programu yako ya WhatsApp hasa kwa watumiaji wa simu za Android.
Hata hivyo baada ya majaribio tumegundua sio kila alama ambayo utaiweka mwenyewe itakuwa na uwezo wa kuharibu programu hiyo bali ni mpaka utumiwe meseji hiyo yenye alama hiyo ambayo ndani yake kuna alama hizo zisizo julikana ambazo zinakuwa ndani ya meseji hiyo mbayo inauwezo wa kuharibu programu yako ya WhatsApp.
Mbali na meseji hiyo, meseji nyingine ambayo inasambaa yenye uwezo wa kuharibu programu ya WhatsApp ni meseji yenye maneno ya “This is very Interesting! ?…Read more” ambayo nayo pia inauwezo wa kuharibu programu yako ya WhatsApp na kufanya programu hiyo kukwama na baadae kuharibika au kucrash. Siku za karibuni kumekua na matatizo mengi kama haya kwani miezi michache iliyopita, tulisikia kuhusu neno la kihindi lenye uwezo wa kuharibu simu za iPhone endapo ukitumiwa kwenye meseji, tatizo ambalo halikuchukua muda Apple walitatua kwa kuleta sasisho jipya la mfumo wa uendeshaji wa simu za iPhone.
Kwa sasa ni vyema kuwa makini na meseji kama hizo na hakikisha hubonyezi alama yoyote unayo ona sio ya kawaida ndani ya meseji hizo. WhatsApp bado haijatoa taarifa zozote kuhusu tatizo hilo lakini bila shaka tatizo hilo lita rekebishwa siku za karibuni.