Kampuni ya Twitter imetangaza kufuta alama ya Verified ya Legacy kuanzia mwezi ujao tarehe moja mwaka huu. Kwa mujibu wa TechCrunch watu wote walio wekewa alama ya Verification hapo awali alama hiyo itafutwa.
Licha ya umuhimu wa siku iliyo chaguliwa na Twitter (Siku ya Wajinga Duniani), kuondolewa kwa alama za verification za zamani kumetarajiwa kwa miezi sasa.
Musk aliandika ujumbe kupitia akaunti yake ya Twitter mwezi Disemba akisema kuwa kampuni hiyo itaondoa alama hizo “baada ya miezi michache” kwa sababu “njia ambayo alama hizo zilitolewa kwa watumiaji ilikuwa isiyo ya haki na yakipumbavu.”
In a few months, we will remove all legacy blue checks. The way in which they were given out was corrupt and nonsensical.
— Elon Musk (@elonmusk) December 12, 2022
Hata hivyo Tangu kipindi hicho hadi sasa wamiliki wa alama ya Verification wamekuwa wakiona ujumbe wanapobonya alama hiyo kuashiria kwamba alama hiyo ni uthibitisho wa zamani na inaweza kuwa muhimu au isiwe muhimu.
Hata hivyo kwa sasa unaweza kununua alama hiyo ya uthibitisho kupitia Twitter Blue kwa $8 au sawa na kati ya TZS 19,000 kwa mwezi pamoja na kodi.
Huku usajili wa iOS na Android utagharimu $11 sawa na TZS 26,000 kwa mwezi, kutokana na gharama za duka la programu yani App Store au Play Store. Twitter Blue kwa sasa inapatikana duniani kote.
Hata hivyo, pia kuna rangi na nembo nyingine za uthibitisho (Verification Badge) ambazo zinapatikana kwa kununuliwa ili kuelezea ikiwa akaunti ni ya biashara au serikali au nyingine yoyote.
Twitter inasema kununua alama ya uthibitisho verification, kutatoa fursa kwa watumiaji kupata huduma za wanachama kama vile kuona matangazo kidogo kwenye timeline, kupewa kipaumbele katika mazungumzo na uwezo wa kuandika maandishi marefu kwenye tweet moja, pamoja na uwezo wa kuhariri au kuedit maandishi na kufuta maandishi kwenye tweet.
Hii inaashiria mtindo mpya wa mitandao ya kijamii na ina wezakana kabisa mtindo huu ukachukuliwa na mitandao mingine kama facebook, pamoja na Instagram hata Tiktok kama njia ya kuongeza mapato ya kampuni hizi.
Kwa sasa Instagram nayo inafanya majaribio ya kuruhusu watumiaji wake kununua alama ya uthibitisho au verification, huku nchi nyingi zaidi zikiwa tayari zipo kwenye majaribio hayo.