Linapokuja swala la kuwa na akaunti za mitandao ya kijamii ni wazi kuwa kila mtu anajua umuhimu wa kuwepo na akaunti hizi. Hivi karibuni kampuni na watu wengi binafsi wamekuwa wanatumia mitandao ya kijamii, kuajiri watu ikiwa pamoja na kuangalia aina ya mtu au watu ambao kampuni au mtu anataka kushirikiana nae kwenye jambo.
Sasa kuliona hili ni muhimu kuwa na akaunti bora za mitandao ya kijamii kwani ni wazi kuwa akaunti zako za mitandao ya kijamii zinaweza kuonyesha wewe ni mtu wa aina gani.
Kuliona hil leo nimekuletea makala ambayo itakusaidia kujua mambo ya muhimu ya kuzingatia ili kuwa na akaunti bora za mitandao ya kijamii au social media.
Kumbuka makala hii imegawanyika kwenye sehemu mbili, yaani mambo muhimu kwa mtu binafsi na mambo muhimu kwa akaunti za kibiashara. Basi bila kupoteza muda twende moja kwa moja kwenye makala hii.
Mambo Muhimu kwa Akaunti Binafsi
Kwa kuanza ningependa ufahamu mambo muhimu ambayo ni bora kwa mtu binafsi. Kumbuka mambo haya ni muhimu kama unataka kuanzisha akaunti kwaajili ya mtu binafsi, lakini pia unaweza kutumia kama wewe binafsi ni mfanya biashara au unatoa huduma fulani.
Hakikisha Unatafuta Jina Sahihi
Jina pekee linatosha kusema mengi kuhusu wewe, ni wazi kuwa ukisikia mtu anaitwa jina la ajabu ni lazima wazo litakujia kuwa kuwa mtu huyo ana tabia kama jina hilo.
Hivyo basi, jina unalo chagua ni muhimu sana liwe jina lako binafsi na kama jina lako halipatikani basi hakikisha unaweka alama nzuri kwenye jina lako.
Alama nzuri ni pamoja na underscore (_), au nukta (.), au unaweza kuchagua neno (iam), (official) au jina lolote ambalo ni bora na lenye kuonyesha utarabu au busara.
Hakikisha unaepuka kutumia majina ambayo sio sahihi au majina ya vitu, mahali au majina ambayo sio rasmi kutumika na watu. Pia usitumie jina linalo fanana sana na mtu mwingine.
Weka DP Bora Yenye Sura Yako
Linapokuja swala la picha ni wazi kuwa watu wengi husahau nguvu ya picha. Picha ni kiungo muhimu sana na ukitumia vibaya inaweza kuharibu maisha yako.
Linapokuja swala la profile picture au DP ni muhimu kuweka picha yako yenye sura yako, hii ni muhimu hasa kama unataka kutengeneza jina lako mbele ya watu mbalimbali.
Ni wazi kuwa baadhi ya makampuni hutumia mitandao ya kijamii kuweza kujua zaidi kuhusu mtu au watu wanao waajiri. Hivyo ni muhimu sana kutumia picha nzuri yenye maadili kwenye DP yako kwani ndio kitu cha kwanza ambacho mtu anaona kabla ya kuangali kwenye ukurasa wako.
Andika Bio Yenye Kueleza Kuhusu Wewe
Moja ya sehemu ya pili ambayo mtu huangalia anapo fungua profile yako yoyote kwenye mtandao wowote wa kijamii ni pamoja na sehemu ya Bio au Biography.
Sehemu hii ni muhimu kwa kuwa ndio yenye kueleza kuhusu wewe pamoja na ukurasa wako au profile yako.
Ni muhimu kandika Bio yenye kutoa maelezo ya wewe ni nani, au unafanya nini. Hii ni muhimu kwa kuwa maelezo yako mwenyewe yanaweza kutoa picha halisi ya wewe ni mtu wa aina gani
Ni vyema kuandika bio yenye maneno mafupi ambayo inaweza kumfanya mtu ajue moja kwa moja kama wewe ni mtu wa aina gani.
Mfano unaweza kuandika “Mtanzania, muandishi wa habari wa kujitemea na mjasiriamali“.
Hii pekee inatosha kuonyesha wewe ni mtu wa aina gani na ni kitu gani ambacho ni muhimu kwenye ukurasa wako na watu wategemee kukutana na nini wanapo tazama ukurasa wako.
Weka Link Kwenye Bio
Link kwenye bio yako ni moja ya kitu muhimu sana, hii ni muhimu kwa kuwa inaweza kusaidia kuweza kutangaza mambo ya muhimu kuhusu wewe.
Unaweza kuweka link ya mitandao ya muhimu ambayo unaonyesha kazi zako zaidi. Lakini pia unaweza kuchagua kuweka link kwenye bio ambayo inaweza kuonyesha kila kitu ikiwa pamoja na akaunti zako za mitandao ya kijamii.
Unaweza Kutengeneza Link Kwenye Bio bure kabisa kwa kubofya hapo Hapa
Mitandao mingi inaruhusu kutengeneza link yako ni bure kabisa na huto chajiwa gharama yoyote. Kama unataka kujifunza zaidi jinsi ya kutumia Bio Link yako unaweza kutembelea hapa kujua tovuti za kutengeneza link kwenye bio.
Kwa kusema hayo, hayo ndio mambo ya muhimu ambayo unatakiwa kuwa kufanya kabla ya kuamua kutengeneza akaunti yoyote ya mitandao ya kijamii.
Makala inayo fuata tutaenda kuangalia mambo ya muhimu kufanya kabla ya kuwa na akaunti ya mitandao ya kijamii kwa ajili ya biashara.