Zaidi ya akaunti milioni 412 za mtandao wa kutafuta marafiki na wapenzi wa FriendFinder zimeripotiwa kuvujishwa na maharamia wa mtandaoni (Hackers), maharamia hao wamevujisha email pamoja na password ambazo zilikusanywa na kampuni hiyo zaidi ya miaka 20 kupitia tovuti yake ya Penthouse.com.
Taarifa kutoka kwenye tovuti ya LeakedSource ambayo ndio iliyo ripoti tukio hilo siku ya jana jumapili zinasema kuwa, akaunti zaidi ya milioni 339 zilizovuja zilitoka kwenye mtandao wa AdultFriendFinder.com, ambao kampuni hiyo hutumia maneno ya “world’s largest sex and swinger community” ikiwa na maana ni mtandao mkubwa zaidi duniani wa kutafuta wapenzi na marafiki.
Uharamia huo unasemekana ulitokea mwezi October mwaka huu (2017) ambapo pia akaunti zaidi ya milioni 15 ambazo zilikua zina aminiwa kufungwa kabisa na watumiaji zilivujishwa pia kwani kampuni hiyo iliendelea kuhifadhi data za watumiaji hao kwenye server zake hata baada ya watumiaji hao kufuta akaunti hizo.
Hata hivyo bado kampuni hiyo ya FriendFinder haijaongelea lolote kuhusu ili ila habari kutoka mtandao wa ZDNet, zinadhibisha kuwa maharamia hao wamevujisha akaunti hizo. Hii sio mara ya kwanza kwa mtandao huo kuwa hacked na maharamia mwaka 2015 kampuni hiyo ilikuwa hacked na akaunti zaidi ya milioni 3.5 zilivujishwa mtandaoni.
Je unasemaje kuhusu hii .? tuandikie maoni yako hapo chini au unaweza kujiunga na majadiliano kwenye mitandao yetu ya kijamii ya Facebook, Twitter na Instagram pamoja na Youtube kama unataka kujifunza mambo mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya Video. Pia kama unataka kupata habari zote za teknolojia kwa haraka unaweza kudownload sasa App yetu ya Tanzania tech kutoka Play Store na hivi karibuni itapatikana kupitia App Store.