Kama wewe ni mtumiaji wa mtandao wa Airtel basi habari njema kwako kwani kampuni hiyo ya simu imetangaza rasmi kuanza kufanya gawio la sh bilioni 2 kwa wateja wake wa Tanzania.
Akitangaza Taarifa hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Sunil Colaso imethibitisha kuwa gawio hilo linatokana na faida waliopata kutokana na huduma za Airtel Money, hivyo wameamua kurudisha kwa wateja wao kama ilivyo kawaida yao.
Hata hivyo Airtel ilianza utaratibu huu toka Mwaka 2015 na hadi kufikia leo hii jumla ya Sh11.8 bilioni zimeshagawiwa kwa wateja wa Airtel Money. Akielezea jinsi wanavyo gawa pesa hizo Sunil alisema “Kila mtumiaji na mteja wa Airtel Money hupata sehemu ya gawio hilo kulingana na salio linalosalia katika akaunti yake ya Airtel Money kila siku”.
Pia mkurugenzi huyo alibainisha kuwa gawio la pesa hizo linatokana na faida iliyopatikana kuanzia mwezi wa sita hadi kufikia mwezi wa kumi mwaka huu 2017. Airtel Money ni moja ya huduma za kifedha ambazo kwa dar es salaam zimekuwa hazitumiki kwa wingi sana ukilinganisha na huduma za mitandao mingine ya simu.
Je nini maoni yako kuhusu hili..? tuandikie kwenye maoni hapo chini. Kwa habari zaidi za teknolojia hakikisha una download App ya Tanzania Tech kupitia Play Store pia usasahau kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech kupitia Youtube ili uweze kupata habari zote za teknolojia kwa njia ya Video.
Thanks Tanzania Tech
Karibu sana