Tanzania Kumiliki Asilimia 49 ya Hisa za Airtel Tanzania

Bado Asilimia 1 ili Tanzania iweze kumiliki nusu ya kampuni ya Airtel Tanzania
Airtel Tanzania kumilikiwa na serikali kwa asilimia 49 Airtel Tanzania kumilikiwa na serikali kwa asilimia 49

Habari kutoka tovuti ya gazeti la kila siku la mwananchi zinasema kuwa, Kampuni ya Bharti Airtel imekubali kuongeza hisa zinazomilikiwa na Serikali ya Tanzania katika kampuni ya Airtel Tanzania kutoka asilimia 40 hadi kufikia asilimia 49.

kwa mujibu wa mwananchi, inasemekana kuwa taarifa ya makubaliano hayo imetoleo leo na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa baada ya mazungumzo kati ya Rais John Magufuli na mwenyekiti wa kampuni ya Bharti Airtel Sunil Mittal, waliokutakana Ikulu jijini Dar es Salaam.

Advertisement

Taarifa hiyo inaeleza kuwa baada ya mazungumzo hayo Mittal amesema kampuni yake imekubali kuongeza hisa zinazomilikiwa na Serikali ya Tanzania katika kampuni ya Airtel Tanzania kutoka asilimia 40 hadi asilimia 49 na kufanya kampuni ya Bharti Airtel kuwa na hisa kutoka asilimia 60 hadi kufikia asilimia 51.

raisi magufuli na mweneyekiuti wa bhati airtel
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisoma taarifa ya majadiliano kutoka kwa mgeni wake Bw. Sunil Mittal Mwenyekiti wa Bharti Airtel ( kampuni ya Simu ya Airtel ) mara baada ya Mazungumzo yao . Ikulu Jijini Dar es Salaam. Januari 11,2019. Picha na Mwananchi

Raisi Magufuli ameelezea kufurahishwa kwake na hatua iliyofikiwa katika mazungumzo hayo na kueleza kuwa Masuala mengine ya kumalizia mazungumzo hayo yataendelea leo ili kumalizia mchakato mzima.

Raisi Magufuli alinukuliwa akisema “Masuala mengine ya kumalizia mazungumzo haya yataendelea leo ili kumalizia, lakini jambo zuri ni kuwa sasa wamekubali kutoa gawio kwa Serikali ambapo kwa muda wa miaka minane hadi kumi tulikuwa hatujapata gawio,” amesema Magufuli.

“Kiasi cha asilimia za gawio nacho watajadili leo, kwa hiyo mimi naona huu ni mwanga mzuri wa kwenda mbele kati ya kampuni ya Bharti Airtel na Serikali ya Tanzania pamoja na kampuni zingine.”

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use