Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Airtel Kuanzisha Maabara ya Kompyuta Hapa Tanzania

Sasa wanafunzi wa kitanzania kuweza kujifunza kompyuta kwa usahihi
Airtel Airtel
PICHA KUTOKA MWANANCHI

Kampuni inayotoa huduma za simu za mkononi ya Airtel hivi karibuni kwa kushirikiana na Atamizi Teknohama ya mjini dar es salaam (DTBi) limemaliza kufanya mafunzo maalumu kwa walimu wa shule za secondary na msingi ikiwa ni katika hali ya kujiandaa kufungua maabara ya kompyuta hapa nchini Tanzania, imeripoti tovuti ya mwanachi.

Mafunzo hayo yataweza kusaidia vijana wa kitanzania kuweza kujifunza kompyuta mapema na kuwa na uwelewa wa ndani zaidi kwenye mfumo mzima wa kompyuta. Hata hivyo mafunzo hayo kwa walimu wa tanzania yametolewa na walimu kutoka kituo cha elimu cha Galway cha nchini Ireland yakiwa na lengo la kuwapa ujuzi walimu hao ili waweze kuwafundisha wanafunzi watakao jiunga au kutembelea maabara hiyo.

Advertisement

Kutokana na changamoto iliyopo sasa ya wanafunzi wengi kutumia kompyuta kwa mara ya kwanza wanapoanza masomo ya chuo kikuu kumefanya kumefanya kuwe na ufinyu katika ubunifu na kutumia teknoloJia katika ujasiriamali. Tunaamini maabara ya Airtel Fursa yatatoa mwanya kwa vijana kujifunza masomo na kuvumbua mambo mengi wakiwa katika umri mdogo.” alisema George Mulamula, Mkurugenzi wa DTBi chini ya COSTECH.

Maabara hiyo ya Airtel Fursa itatatoa fursa kwa vijana wenye malengo ya kujifunza masomo ya tehama kuongeza ujuzi na kutoa mwanga kwa vijana kuwa wabunifu kwa kuzindua ‘application’ mbalimbali ambazo zitaweza kuwaingizia kipato.

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya video.

Habari Kutoka : Mwananchi

5 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use