Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Airtel Kenya Yaondoa Gharama Zote za Kutuma Pesa

Gharama hizo zitaondolewa kwa muda wa siku 90 kuanzia leo
Airtel Kenya Yaondoa Gharama Zote za Kutuma Pesa Airtel Kenya Yaondoa Gharama Zote za Kutuma Pesa

Kutokana na kuendelea kusambaa kwa virusi vya corona (CODIV-19), kampuni ya kutoa huduma za mawasiliano ya Airtel ya nchini Kenya, imetangaza kuondoa gharama za kutuma pesa kwa watumiaji wa Airtel Money nchini humo.

Hatua hii inakuja siku chache baada ya Raisi wa Kenya, Uhuru Kenyatta, kutangaza kuwa kampuni za simu na mabenki nchini Kenya kuangalia njia za kuongeza matumizi ya pesa kupitia simu ili kupunguza maambukizi ya virusi vya corona (CODIV-19).

Advertisement

Tofauti na kampuni ya Safaricom iliyotangaza kuondoa gharama kwa watumiaji wa M-Pesa watakao tuma pesa kuanzia Ksh 1000, kwa mujibu wa tovuti ya The East African, Airtel imetangaza kuondoa gharama zote za kutuma pesa kwa watumiaji wa kiwango chochote cha pesa kuanzia siku ya leo tarehe 17 Machi hadi hapo zitakapo kamilika siku 90.

Mbali na hayo kampuni ya Airtel ya nchini Kenya imeongeza kikomo cha kutuma Pesa kupitia Airtel Money kutoka Ksh 70,000 (TZS 1,600,000) hadi Ksh 150,000 (TZS 3,300,000) wakati kikomo cha kila siku cha shughuli za pesa kimeongezwa hadi kufikia Ksh 300,000 (6,600,000) kutoka Ksh 140,000 (TZS 3,100,000).

Kwa upande wa hapa nchini Tanzania, hadi kufikia siku ya leo tarehe 17 mwezi machi 2020, mgonjwa mmoja tu ndio aliye tambulika kuwa na virusi vya corona. Hata hivyo, kwa mujibu wa tovuti ya Mwananchi tayari serikali ya Tanzania imechukua hatua ya kuzifunga shule zote za awali, msingi na sekondari kwa siku 30 kuanzia leo Jumanne Machi 17, 2020 ili kuzuia kusambaa kwa maambukizi ya virusi vya Corona (CODIV-19).

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use