Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

WhatsApp Yaleta Aina Mpya ya Status za Maandishi na Rangi

Sasa sio picha pekee sasa unaweza kuweka maneno na rangi
WhatsApp Yaleta Aina Mpya ya Status za Maandishi na Rangi WhatsApp Yaleta Aina Mpya ya Status za Maandishi na Rangi

Hivi leo WhatsApp imetangaza kuleta aina mpya ya status kwenye programu yake ya WhatsApp, aina hiyo mpya sasa inakuwezesha kuweza kuweka maneno pamoja na rangi kwa nyumba huku ukiwa na uwezo wa kuchagua font au mwandiko unao taka.

Kwa mujibu wa tovuti ya thenextweb sehemu hiyo mpya itakuwa na uwezo pia wa kuweza kuonyesha link ambayo mtu aki bofya atapelekwa kwenye tovuti husika. Haidha sehemu hiyo mpya inategemewa kuanza kutoka kuanzia leo kwa watumiaji wote wa programu hiyo wa iOS, Android pamoja na watumiaji wa programu hiyo kwenye kompyuta.

WhatsApp status imeonekana kuwa sehemu maarufu sana baada ya kuzinduliwa mapema mwaka huu, ikiwa ina ongezeko kubwa sana la watumiaji wa sehemu hiyo ambayo imekuwa kama chai asubuhi kwani kila siku ni lazima upitie hapo kuangalia yaliyomo au kubadilisha Status hizo kutokana na tabia yake ya kudumu ndani ya masaa 24 tu…

Kama bado ujaipata njia hii mpya basi endelea kusubiri uku ukiangalia update za programu ya WhatsApp kupitia masoko ya Play Store pamoja na App Store.

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya Video.

Chanzo : The Next Web

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use