Kwa mujibu wa tovuti ya The Citizen, Hivi sasa watanzania wanaweza kutathmini kwa urahisi na kwa usalama dalili za Covid-19 kwa kutumia njia mpya wakiwa nyumbani, shukrani kwa mpango mpya wa Huduma ya Afya ya Aga Khan na Chuo Kikuu cha Aga Khan (AKU).
Kwa mujibu wa tovuti hiyo, Asasi hizo mbili zimezindua programu mpya ya Android na iPhone ambayo inaruhusu watu kutathmini kwa urahisi dalili za Covid-19 wakiwa nyumbani na kwa hivyo, kujua hatua zifuatazo baada ya kujua afya yao. App hiyo iliyopewa jina la CoronaCheck, inaweza kupakuliwa kwenye soko la Play Store na App Store bila Malipo yoyote.
Kupitia app hiyo ambayo ipo kwa lugha ya Kiswahili na Kiingereza, utaweza kujibu maswali mbalimbali kuhusu afya yako ikiwa pamoja na kueleza kama unajisikia dalili za tofauti katika mwili wako. Pia kupitia app hiyo utaweza kupata vidokezo vya muhimu kuhusu virusi vya corona, pamoja na kupata namba za dharura za kutoa taarifa kuhusu COVID-19.
Programu hiyo ni ya kwanza kwa hapa Tanzania, lakini sio programu ya kwanza ambayo inatoa nafasi ya kuelimisha kuhusu virusi vya corona. Wiki chache zilizopita, pia serikali ya Australia ilizindua app maalum ya kusaidia kutambua kwa urahisi walio ambukizwa virusi vya corona iliyokuwa inaitwa CovidSafe.
Kwa sasa kama upo hapa Tanzania unaweza kupata app hii mpya ya Corona Check kupitia masoko ya Play Store au App Store au kama link hizo hazifanyi kazi unaweza kubofya link hapo chini.
CoronaCheck – Android
CoronaCheck – iOS