Kampuni ya Adobe imetangaza kuzindua programu yake mpya inayoitwa Project Rush, programu hii ni maalum kwaajili ya kuedit video na inakuja ikiwa na uwezo wa kutumika kwenye vifaa vyote, yaani kompyuta pamoja na kwenye simu za mkononi (smartphone).
Tofauti na programu zingine za Adobe za kuhariri video kama vile Premiere Pro, programu hii mpya ya Project Rush inakuja ikiwa ni rahisi kutumia na ikiwa imewezeshwa kupatikana kwenye vifaa vya mifumo yote ya Windows, Mac, Android pamoja na iOS.
Mbali na hayo programu hiyo inakuja ikiwa inatumia teknolojia zinazo fanana na programu za Premiere Pro, pamoja na After Effects, lakini Project Rush yenyewe itakuja ikiwa na uwezo wa kuhariri baadhi ya vitu kama vile rangi, video, sauti pamoja na vitu vingine vidogo vidogo. Tofauti na hayo programu hiyo ya Project Rush inakuja na njia mpya ambayo unaweza kuitumia kusambaza video zako baada ya kuhariri kwenda kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii, kama vile YouTube, Facebook au hata Instagram.
Programu hii mpya inatarajiwa kutoka rasmi baadae mwaka huu, lakini unaweza kuanza kuitumia sasa kama sehemu ya majaribio, Kujiunga bofya hapa kisha bofya sehemu iliyoandikwa Apply na kisha jaza fomu na hapo utakuwa umejiunga na programu hiyo ya majaribio na utaweza kujaribu sehemu za programu hiyo kabla haijatoka rasmi hapo tarehe 23 mwezi june mwaka huu 2018.