Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Achana na Instagram, Spotify Tumia App Hizi Badala Yake

Tumia app hizi kuweza kupakua picha, video na muziki moja kwa moja
Achana na Instagram, Spotify Tumia App Hizi Badala Yake Achana na Instagram, Spotify Tumia App Hizi Badala Yake

Katika ulimwengu wa sasa ni wazi kuwa kila mtu anataka kufanya zaidi, Smartphone zimetupa uwezo wa kufanya mambo mengi lakini baadhi ya apps bado zinakuja na vikwazo mbalimbali ambavyo unaweza kuepuka kama unahitaji.

Kupitia makala hii nitaenda kuonyesha apps mbili ambazo unaweza kutumia badala ya App ya Instagram pamoja na app ambayo unaweza kutumia badala ya Spotify.

Advertisement

Kizuri ni kuwa huna haja ya kuondoa app ya Instagram au Spotify kwenye simu yako bali unaweza kutumia apps hizi zote moja kwa moja kwenye simu yako zikiwa sambamba na app za Instagram na hata Spotify.

Mbadala wa App ya Instagram

Kama kwa namna yoyote umekuwa ukitaka kupakua picha za instagram au video ikiwa pamoja na kuangalia profile picture za watu kwa ukubwa ikiwa pamoja na kuondoa matangazo na mambo mengine mengi basi utafurahia app hii.

App hii ni copy ya instagram na inakupa uwezo wa kupakua picha, video au kuangalia akaunti ambazo zipo “private” moja kwa moja. Unachotakiwa kufanya ni kupakua app hiyo kisha moja kwa moja install kwenye simu yako ya Android, baada ya hapo hakikisha unatumia username na password ya akaunti ambayo sio muhimu sana kwako ikiwezekana tengeneza akaunti mpya.

Kisha ingia kwenye app hii na akaunti yako hiyo mpya na sasa utaweza kufanya mambo mbalimbali kwa urahisi na haraka. App hii mimi natumia kwa muda sasa na ukweli its the best app for me.

Achana na Instagram, Spotify Tumia App Hizi Badala Yake

Kama unavyoweza kuona utaweza kupakua reels, stories, video au picha yoyote kwa kubofya kitufe cha download. Pia utaweza kuangalia na kudownload profile picture ya mtu yoyote kwa ukubwa kwa kushikilia profile picture hiyo.

Achana na Instagram, Spotify Tumia App Hizi Badala Yake

Mbali na hayo utaweza kufanya mambo mengine mengi zaidi, jaribu app hii na uhakika utakuwa unaitumia kila mara unapotaka kudownload picha au video yoyote kwenye mtandao wa Instagram.

Download Mbadala wa Instagram Hapa

Mbadala wa App ya Spotify

Ni wazi kuwa wengi wetu tunapenda muziki na kwa kuwa tunajua kuwa mtandao wa spotify ni moja ya mitandao bora ya kusikiliza muziki ni wazi hadi sasa kila mtu tayari anayo app ya spotify kwenye simu yake.

Lakini ni wazi kuwa app ya Spotify inakupa uwezo wa kusikiliza muziki lakini huwezi kupakua nyimbo yoyote na hadi ulipie.Hapo mbadala wa app hii ndipo unapokujua.

Achana na Instagram, Spotify Tumia App Hizi Badala Yake

Kupitia app hii utaweza kupakua nyimbo yoyote na kubaki nayo kwenye simu yako moja kwa moja, hii ikiwa pamoja na nyimbo za nje ya nchi pamoja na Playlist kubwa duniani.

Unachotakiwa kufanya ni kutafuta jina la nyimbo na moja kwa moja utaweza kupakua nyimbo hiyo moja kwa moja, mbali na hayo utaweza kupakua nyimbo kutoka mtandao wa YouTube moja kwa moja.

Achana na Instagram, Spotify Tumia App Hizi Badala Yake

Unaweza kupakua nyimbo kutoka nchi mbalimbali kwa kuhakikisha unachagua United States mwanzo wakati wa kufanya setup ya app hii. Pia tumia sehemu ya kutafuta kutafuta nyimbo husika.

Download Mbadala wa Spotify Hapa

Kama kwa namna yoyote unatafuta nyimbo ya Tanzania basi unaweza kutumia tovuti ya nyimbompya kwaajili ya kutafuta nyimbo za Tanzania Tembelea tovuti hii hapa.

Na hizo ndio apps ambazo unaweza kutumia kama mbadala wa app ya Instagram pamoja na app ya Spotify. Kama unataka mbadala wa app nyingine basi endelea kutembelea Tanzania Tech kila siku tuna ahidi kutafuta app nyingine bora kwaajili yako.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use