Acer Yatangaza Laptop Mpya ya Bei Nafuu ya Acer Chromebook 15

Kampuni ya Acer imetangaza laptop yake ya bei rahisi ambayo inauzwa dollar za marekani $199
Acer Chromebook 15 Acer Chromebook 15

Kampuni maarufu ya utengenezaji wa kompyuta ya nchini Taiwan, Acer leo imetangaza kuzindua laptop yake ya bei nafuu ambayo pengine kila mteja ataweza kununua. Laptop hiyo ambayo inauzwa kwa kati ya dollar za marekani $199 mpaka $200 inasemekana ndio laptop ya bei nafuu kwa sasa kutoka kampuni hiyo ya teknolojia.

Mbali na kuwa ni kompyuta ya bei rahisi, Acer Chromebook 15 inatumia mfumo wa undeshaji wa Chrome OS ambao mfumo huu unakuwezesha kutumia programu kama zile zilizoko kwenye simu yako ya Android ikiwa ni pamoja na kucheza michezo (Game) mbalimbali ambazo zinapatikana kwenye mfumo mzima wa Android. Kompyuta hiyo inauwezo wa kutumika vizuri zaidi kama wewe ni mpenzi wa mtandao (Internet) pamoja na kutumia kwa kazi zingine ndogondogo.

Advertisement

Kuhusu sifa za kompyuta hiyo mpya ya Acer Chromebook 15 inasemekana kuwa na sifa za kawaida kwa matumizi ya kawaida kama vile Kioo cha inch 15.6- 1366×768, RAM 2GB, ukubwa wa 16GB Memory ambazo unaweza kutumia Memory Card kuziongeza, sehemu za kuweka flash 2 USB 3.0 Ports, pamoja na sehemu 1 ya kutumia HDMI (HDMI Port). Kwa upande wa battery laptop hii ya Acer Chromebook 15 inasemekana inauwezo wa kudumu na chaji zaidi ya masaa 12 ikiwa ni moja kati ya laptop zinazo kaa na chaji kutoka kampuni hiyo ya Acer yenye makao yake makuu huko New Taipei nchini Taiwan.

Kama umeipenda laptop hiyo na unataka kuinunua unaweza kuinunua kupitia masoko mbalimbali ya mtandaoni ambapo inauzwa kwa kati ya dollar za marekani $235 hadi $249 pia unaweza kuinunua kupitia Amazon.com ambapo pia inauzwa kwa dollar za marekani $249 ambayo ni sawa na shilingi za kitanzania Tsh 545,310.00 kwa mojibu wa viwango vya kubadilisha fedha vya leo tarehe 18-10-2016. 

Kama unataka kujua ni wapi unaweza kuipata laptop hii kwa bei nafuu hapa Tanzania basi endelea kutembelea blog ya Tanzania tech kila siku au unaweza kupata habari zote za teknolojia moja kwa moja kwenye simu yako ya mkononi kwa ku-download App ya Tanzania tech  kwenye simu yako ya Android, au unaweza kujiunga nasi kwa barua pepe pamoja na mitandao yetu ya kijamii ya Facebook, Twitter, Instagram pamoja na Yotube  ili kupata habari mbalimbali za teknolojia pamoja na kujifunza mambo ya teknolojia kwa njia ya video.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use