Habari za jumapili wapenzi wa teknolojia na wasomaji wa Tanzania Tech, leo ni jumapili ya tarehe 21 mwezi may na mwezi kama huu ndio mtandao wa 4G ulipo zinduliwa rasmi kwa hapa Tanzania na mpaka sasa mtandao huo ndio unatimiza rasmi mwaka mmoja.
Katika swala zima la maendeleo na maboresho ya internet nimejikuta nikijiuliza maswali mengi sana na moja ya maswali hayo ni hilo hapo juu kwenye kichwa cha habari. Nimejiuliza hivi kuanzia 4G imeanza mpaka sasa ni takribani mwaka na siku kadhaa hivi kuna mabadiliko yoyote kwenye upande wa speed ya internet.?, Kwa upande wangu nimejikuta nikikosa majibu kwa sababu mbalimbali na sababu hizo ndio zimefanya nilete swali hili kwenu ili muweze kunisaidia jinsi mnavyona kuhusu mfumo huo mpya wa 4G ulianza kutumia rasmi hapa tanzania mwaka 2016.
Nengependa kupata majibu ya ndio au hapana lakini pia ningependa kupata sababu za kwanini unasema ndio au hapana, unaweza kuandika sababu zako kupitia maoni hapo chini nasi tutayapitia moja kwa moja na pengine kuyasogeza maoni hayo kwa wahusika ili waweze kuboresha au kufanya marekebisho ya mambo mbalimbali yanayohusu mtandao wa 4G.
[totalpoll id=”10825″]Kama unatumia programu ya simu ya Tanzania Tech unaweza kutumia link hii https://tanzaniatech.one/-fTJ kutoa maoni yako.
Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya video.
nataka kuwaambiya kwamba app yenu mbona inamatangazo sana mpaka sas hayo matangazo yanaboa
habar zenu