Mmiliki wa kampuni ya X au Twitter Elon Musk, hivi karibuni ametangaza ujio wa mfumo mpya wa akili bandia ambao utakuwa unaitwa xAI Grok.
Mfumo huu ni utakuwa ni mbadala mshindani wa ChatGPT ambayo inatumia lugha model ya GPT (Generative Pre-trained Transformer) na Google Bard, ambayo inatumia Pathways Language Model 2 (PaLM 2).
Announcing Grok!
Grok is an AI modeled after the Hitchhiker’s Guide to the Galaxy, so intended to answer almost anything and, far harder, even suggest what questions to ask!
Grok is designed to answer questions with a bit of wit and has a rebellious streak, so please don’t use…
— xAI (@xai) November 5, 2023
Kwa mujibu wa Elon Musk, mfumo wa xAI Grok, unakuja na maboresho mbalimbali kama vile uwezo wa kutoa majibu ambayo mfumo wa ChatGPT au Google Bard haziwezi kutoa. Pia mfumo huo wa akili bandia utakuwa na data mpya ambazo zitakuwa zinatoka kwenye mtandao wa X.
Mfumo wa Grok AI utakuwa unaweza kujibu maswali mbalimbali, na utakuwa ni mfumo wa akili bandia (AI) ambao unajibu maswali kwa kuchangamka, kuchekesha na ukiwa na uwezo wa kufanya utani na mwanadamu. Pia utakuwa na uwezo wa kutumia mfumo huu, mara nyingi kwa wakati mmoja bila kuzidiwa.
Elon amesema tofauti kubwa kati ya Grok na Akili Bandia nyingine kama vile ChatGPT na Google Bard ni kuwa, Grok ina uwezo mkubwa wa kujibu maswali kwa uchangamfu huku ikiweka utani kidogo.
Kwa sasa kwa mujibu wa Elon Musk, mfumo wa AI ya Grok utaanza kupatikana kwanza kwa watumiaji ambao wanalipia kifurushi cha Premium+ katika mtandao wa X au Twitter. Pia unaweza kujiunga kusubiri ili kuwa wa kwanza kujaribu mfumo huu kupitia link hapa.