Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Simu Mpya za iPhone 15 Pro na 15 Pro Max (Mabadiko Muhimu)

Fahamu mabadiliko muhimu kwenye simu mpya za iPhone 15 Pro na 15 Pro Max
Simu Mpya za iPhone 15 Pro na 15 Pro Max (Mabadiko Muhimu) Simu Mpya za iPhone 15 Pro na 15 Pro Max (Mabadiko Muhimu)

Hatimaye kampuni ya Apple imezindua rasmi matoleo mapya ya simu zake za iPhone 15, na moja kwa moja twende nikujuze yote ya muhimu kwenye simu hizi tukianza na matoleo ya iPhone 15 Pro na iPhone 15 Pro Max.

Advertisement

Muundo

Kwa kuanza na muundao simu mpya za iPhone 15 Pro na 15 Pro Max zinakuja na muundo mpya ambao unakuja na mikunjo huku ikiwa na mikunjo yenye wembamba zaidi kuliko iPhone zote ambazo zimewahi kutoka hadi sasa. Pia uwiano wa simu hii umepunguzwa japokuwa simu hizi bado zina kioo kikubwa vilevile.

Pia kampuni ya Apple imebadilisha fremu za simu hizi kutoka kutengenezwa kwa kutumia Stainless steel hadi sasa kutumia Titanium ambayo hii ni ngumu zaidi na haichubuki kwa wepesi. Pia Apple inadai kuwa simu hii itakuwa nyepesi zaidi kuliko simu zote za iPhone huku ikipungua karibu gramu 19 kutoka simu za iPhone 14 za mwaka jana.

Simu Mpya za iPhone 15 Pro na 15 Pro Max (Mabadiko Muhimu)

Mbali na hayo yote kampuni ya Apple pia imefanya mabadiliko ya swichi ya kuzima sauti au (mute switch) ambayo sasa imebadilishwa na kuwa kitufe badala ya switch.

Simu Mpya za iPhone 15 Pro na 15 Pro Max (Mabadiko Muhimu)

Kupitia kitufe hicho mtumiaji ataweza kuzima sauti kama awali na kufanya mambo mengine mbalimbali kama kupiga picha, kuwasha baadhi ya apps na mengine mengi kupitia sehemu hiyo.

Simu Mpya za iPhone 15 Pro na 15 Pro Max (Mabadiko Muhimu)

Kioo

Kwa upande wa kioo iPhone 15 Pro na 15 Pro Max zinakuja Dynamic Island na Ceramic Shield glass kama ilivyo matoleo ya iPhone 14 Pro, pia ukubwa wa kioo hauja badilika kwani kinakuja na ukubwa wa inch 6.1 huku kikiwa na teknolojia za Super Retina XDR OLED, pamoja na adaptive 120Hz (ProMotion) refresh rate, HDR10, Dolby Vision, pamoja na uwezo wa kuonyesha mwanga hadi nits 2,000 (Hii husaidia zaidi pale unapo angalia simu kwenye jua kali).

Simu Mpya za iPhone 15 Pro na 15 Pro Max (Mabadiko Muhimu)

Kamera

Kwa upande wa kamera iPhone 15 Pro na Pro Max zimekuja na mabadiliko makubwa ambapo sasa zinakuja na kamera kuu ya Megapixel 48MP ambayo inakuja na sensor kubwa ya 1.22µm yenye teknolojia za pre-binned pixels pamoja na toleo jipya la pili la sensor-shift stabilization. Hii inasaidia kuchukua picha za HEIF pamoja na picha za ProRAW kwa pamoja. Pia utaweza kuchagua digital zoom mode kati ya 28mm, 35mm, na 48mm.

Simu Mpya za iPhone 15 Pro na 15 Pro Max (Mabadiko Muhimu)

Kwa upande wa iPhone 15 Pro Max yenyewe inakuja na uwezo mkubwa wa kuzoom hadi 5x tofauti na iPhone 15 Pro ambayo ina zoom hadi mara 3x.

Kamera nyingine za iPhone 15 Pro na 15 Pro Max zinakuja na uwezo wa 12 MP, f/2.8, 77mm ( Kwa telephoto), 12 MP, f/2.2, 13mm, 120˚ ( Kwa ultrawide). Pamoja na TOF 3D LiDAR scanner (depth). Kwa mujibu wa Apple, kamera za simu hizi kwa pamoja zinauwezo wa kushoot movie nzima iliyopo kwenye format ya 4K.

Simu Mpya za iPhone 15 Pro na 15 Pro Max (Mabadiko Muhimu)

Kamera ya mbele inakuja na Megapixel 12, f/1.9, 23mm ( Ambyo ni wide), huku ikisaidiwa na SL 3D, (depth/biometrics sensor) pamoja na teknolojia za HDR, Cinematic mode (4K@24/30fps) huku ikiwa na uwezo wa kuchukua video za hadi 4K@24/25/30/60fps, na 1080p@25/30/60/120fps, gyro-EIS.

Sifa za Ndani

Kwa upande wa sifa za ndani iPhone 15 Pro na 15 Pro Max zinakuja na Chipset mpya ya Apple A17 Pro (3 nm) yenye uwezo wa hadi Hexa-core (2x + 4x). Kwa upande wa GPU zimu hizi zinakuja na uwezo wa graphic mkubwa kiasi kwamba unaweza kucheza game za PS4 kama Resident Evil 4 Remake, na Assassin’s Creed Mirage ambazo zitapatikana baadae mwaka huu. Yote hayo yana wezeshwa na Apple GPU (6-core graphics).

Simu Mpya za iPhone 15 Pro na 15 Pro Max (Mabadiko Muhimu)

Uhifadhi (Storage) na RAM

Kwa upande wa uhifadhi iPhone 15 Pro Max inatarajiwa kupatikana kuanzia GB 256, GB 512 na TB 1, huku 15 Pro ikipatikana kuanzia GB 128, GB 256, GB 512 na TB 1.Kwa upande wa RAM bado hadi sasa hakuna ripoti kamili simu hizi zinakuja na RAM kiasi gani, lakini tegemea kuanzia RAM GB 6 na kuendelea.

Viunganishi

Kwa upande wa viunganishi mabadiliko makubwa yapo kwenye waya wa kuchaji pamoja na data ambao sasa iPhone zote ikiwa pamoja na iPhone 15 Pro na Pro Max zitakuwa zinatumia USB Type C (USB C).

Simu Mpya za iPhone 15 Pro na 15 Pro Max (Mabadiko Muhimu)

Hii ina maanisha kuwa utaweza kuchaji simu yako kwa urahisi kwa kutumia chaji ya USB Type C ambayo unatumia kwenye simu yako ya Android.

Bei na Upatikanaji

Kwa upande wa bei bado hakuna bei rasmi kwa hapa Tanzania lakini kwa mujibu wa Apple simu ya iPhone 15 Pro Max itapatikana kuanzia dollar $1199 sawa na takribani TZS 3,010,000 kwa GB 256, huku iPhone 15 Pro ikipatikana kuanzia $999 sawa na takribani TZS 2,510,000 kwa GB 128. Kutokana na uwadimu wa dollar nchini kwetu tegemea simu hii kupatikana kwa zaidi ya TZS 4,000,000 kwa toleo la Pro Max.

Simu Mpya za iPhone 15 Pro na 15 Pro Max (Mabadiko Muhimu)

Battery

Kwa mujibu wa Apple, Battery za iPhone 15 Pro na Pro Max zote zimeongezwa uwezo na sasa zitakuwa zinadumu na chaji zaidi huku ikisemekana kuwa na uweza wa kudumu na chaji siku nzima bila kuchaji. Kwa upande wa Size ya Battery ya simu hizi hadi sasa bado Apple hawajaweka wazi kuhusu hilo.

Na hayo ndio machache kuhusu simu mpya za iPhone 15 Pro na iPhone 15 Pro Max, kama unataka kujua zaidi kuhusu simu za iPhone 15 na iPhone 15 Plus basi unaweza kusoma makala yetu ijayo. Kwa habari zaidi za teknolojia pakua app yetu ya Tanzania Tech Hapa.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use