Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Namba Mbili Ndani ya Programu Moja ya WhatsApp!

Maboresho ya hivi karibuni tokea WhatsApp
Namba Mbili Ndani ya Programu Moja ya WhatsApp! Namba Mbili Ndani ya Programu Moja ya WhatsApp!

Kwa muda mrefu, namna ya kutumia namba mbili za mtu binafsi katika WhatsApp ilikuwa kupitia kutumia programu za WhasApp na WhatsApp Business kwa pamoja ama kutumia nyenzo za kimfumo kama Dual Messenger ili kuifanya simu kufungua programu pacha ya WhatsApp na kuweza kusajili namba nyingine.

Hilo linabadilika sasa, ambapo WhatsApp wameiongezea uwezo programu yao kuweza kutumia akaunti mbili kwa mpigo, yaani kuwa na namba mbili za Whatsapp zitakazofunguka kwa programu hiohio moja ya WhatsApp.

Advertisement

Namba Mbili Ndani ya Programu Moja ya WhatsApp!

Mtumiaji sasa ataweza kusajili namba yake ya siku zote, na kuweka nyingine kama akaunti nyongeza, kama ambavyo unaweza kuongeza anwani ya barua pepe kwenye simu ama kompyuta.

WhatsApp wanakuwa ni mtandao mwingine unaaongeza uwezo huo katika programu yake, ikifuata mitandao kama Telegram ambao imekuwa na uwezo huo kwa muda sasa. Sasa, itakuwa rahisi kwa watumiaji wenye namba zaidi ya moja zilizosajiliwa WhatsApp kuweza kutumia namba hizo zote na kutazama jumbe wanazopata kwa urahisi zaidi.

Katika mabadiliko haya, WhatsApp pia wamebadili mwonekano wa programu yao katika simu za Android, ambapo sasa vitufe kwa ajili ya kuchagua Chats ama Status na kadhalika vimehamishiwa chini, kama ilivyo katika Simu za Apple.

Namba Mbili Ndani ya Programu Moja ya WhatsApp!

Pale Juu, neno WhatsApp limebaki kama kawaida,na vitufe baadhi vya mfumo lakini wameongeza sehemu ya kufungua taarifa zako binafsi (Profile) moja kwa moja. Sasa ni kitufe ambacho muda wote kinaonesha picha ya utambuzi wako uliyoiweka. Ukipagusa hapo kwa sekunde kadhaa, WhatsApp itafungua sehemu ambapo utaweza kuingia katika akaunti nyingine, ama namba nyingine uliyoisajili palepale. Kama hujaiongeza bado, itakupa uwezo huo wa kuongeza.

Huu ni mwendelezo wa maboresho ambayo WhatsApp inafanya katika programu na mfumo wao ili kuboresha matumizi ya mtandao huo wenye watumiaji wengi sana duniani.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use