Mtandao wa WhatsApp katika maboresho ya hivi karibuni, wameongeza uwezo wa watumiaji wake kutuma picha zenye ubora mkubwa, wakiziita kama “HD Pictures“.
Hapo awali, Whatsapp ilikuwa ikipunguza ukubwa na ubora wa picha moja kwa moja wakati wa kuituma au kuisambaza ili kutumia kiasi kidogo cha data.
Ukubwa wa picha hapo kabla ulikuwa ukizuiwa kuwa 1600 x 1052, na kufanya picha zenye ubora zaidi ya hapo kupungua ubora. Hivi sasa, whatsapp wameongeza uwezo wa kutuma picha hadi kiasi cha 4096 x 2692, hii ikiwa ni ongezeko kubwa la ubora. Hii itamaanisha pia, picha hizo zitatumia data zaidi.
Sasa, mtumiaji atakuwa na uwezo wa kutuma picha kwa mfumo wa awali wenye ubora mdogo ama kutuma picha za HD zenye ubora mkubwa.
Mtumiaji ataweza kubadili ubora wa picha kwa chaguzi rahisi akiwa anatuma picha hiyo. Hii imeanza kwa upande wa picha lakini Whatsapp wanatarajiwa kuongeza uwezo huu kwa video pia, hivyo kuwa na uwezo wa mitandao kama Telegram ya kutuma taarifa kwa ubora mkubwa kiasili, bila kuzipunguza ubora ndani kwa ndani na kumfanya mtumiaji kuwa na chaguzi hizo.
Chanzo: GSMArena, Wabetainfo