Threads, programu mpya iliyotolewa na kampuni ya Meta au (Facebook Zamani), imepokelewa kwa shangwe na mamilioni ya watumiaji ndani ya masaa yake ya kwanza saba. Kwa kuwa programu hii inalenga kuwa mpinzani “rafiki” wa Twitter, ina uwezo wa kuvutia watumiaji ambao hawaridhishwi na mabadiliko ya hivi karibuni kwenye jukwaa hilo.
Ikiwa wewe ni mmoja wa watu hao ambao wanapenda kujaribu Threads, hapa kuna mwongozo wa hatua kwa hatua wa jinsi ya kuunda akaunti yako ya Threads.
TABLE OF CONTENTS
Hatua ya 1: Pakua Programu ya Threads
Kwanza kabisa, ingia kwenye duka la programu la simu yako, kama vile Google Play Store kwa Android au App Store kwa iOS. Tafuta programu ya Threads na uipakue kwenye simu yako. Baada ya kupakua na kusakinisha, fungua programu ya Threads.
App ya Threads Android
App ya Threads iOS
Hatua ya 2: Ingia Kwa Kutumia Akaunti ya Instagram:
Threads ni programu iliyoundwa kwa ushirikiano na Instagram, kwa hivyo itakuhitaji kuingia kwa kutumia akaunti yako ya Instagram. Chagua chaguo la “Ingia na Instagram” kisha moja kwa moja ingia kwenye akaunti yako ya Instagram kisha angalia sehemu ya Notification kisha chagua sehemu ya Notification inayoonyesha kuna mtu ameingia kwenye akaunti yako kisha bofya Approve
Baada ya hatua hiyo rudi kwenye app ya Threads na moja kwa moja utaunganishwa na akaunti yako ya Instagram na kuwa tayari kuanza kutumia Threads.
Hatua ya 3: Kubadilisha Wasifu Wako:
Baada ya kuingia kwenye Threads, utaona kwamba jina lako la mtumiaji wa Instagram limehamishiwa moja kwa moja. Ikiwa unataka, unaweza kuhamisha wasifu wako kutoka Instagram kuja Threads. Lakini pia unaweza kuedit Bio yako na profile picture, Chagua chaguo la “Badilisha Profile” na ufuate maelekezo ya kuongeza picha ya wasifu au kufanya mabadiliko mengine kulingana na mapendekezo yako.
Lakini kama unataka bofya sehemu ya Import from Instagram kuweza kuhamisha wasifu wako wa instagram kuja kwenye app ya Threads.
Hatua ya 4: Kufuata Watumiaji na Kuunda “Threads”:
Sasa umewekwa kwenye programu ya Threads na tayari kuanza kuunda “threads” zako. Unaweza kufuata watu wanaotumia Instagram sawa na vile unavyofanya kwenye Instagram. Tafuta watu kwa jina la mtumiaji, jina halisi au kwa kupitia orodha ya mapendekezo. Kisha chagua “Fuatisha au Follow” ili kuwa na mwendelezo wa machapisho yao kwenye ukurasa wako wa “threads”. Pia, unaweza kuunda “threads” zako kwa kubonyeza kitufe cha “Tuma Ujumbe” na kuandika ujumbe wako wa hadhira.
Tofauti Kati ya Twitter na Threads
Kwa sasa unaweza kuona tofauti kati ya Twitter na Threads na jinsi ambayo imeweza kufanana na mtandao wa Twitter.
Hitimisho
Kwa kufuata mwongozo huu wa hatua kwa hatua utakusaidia kuunda akaunti ya Threads na kuanza kutumia programu hiyo. Tafadhali kumbuka kuwa Threads inahitaji akaunti ya Instagram ili kuingia. Fuata hatua hizi na ujiunge na jukwaa la Threads ili kuwa sehemu ya watumiaji wa kwanza wa mtandao huu wa Threads.