Jinsi ya Kutumia Google Bard, Mfumo wa AI Kama ChatGPT

Fahamu jinsi ya kuanza kutumia mfumo wa AI wa Google Bard
Jinsi ya Kutumia Google Bard, Mfumo wa AI Kama ChatGPT Jinsi ya Kutumia Google Bard, Mfumo wa AI Kama ChatGPT

Kwa sasa huduma za AI zimeonekana kuiteka dunia kwa kiwango kikubwa, hii ni baada ya kampuni ya OpenAI kuanzisha mfumo wa ChatGPT, zipo kampuni nyingi sana ambazo kwa sasa zimejikita kwenye utengenezaji wa huduma zinazotumiwa mfumo wa AI kurahisisha huduma zake moja ya kampuni hizo ni kampuni ya Google ambayo inakuja na mfumo wa Google Bard ambao unafanana na ChatGPT.

Google Bard ni Nini?

Google Bard ni huduma ya mfumo wa AI ya Google. Huduma hii inalenga kufanya kazi kwa njia sawa na ChatGPT, tofauti kubwa ikiwa ni kwamba Google Bard inapata data zake kutoka mtandaoni au kupitia wavuti mbalimbali.

Advertisement

Jinsi ya Kutumia Google Bard, Mfumo wa AI Kama ChatGPT

Lini Google Bard ilianzishwa?

Bard ilizinduliwa tarehe 6 Februari kupitia taarifa kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Google na Alphabet, Sundar Pichai. Ingawa Bard ilikuwa ni wazo jipya kabisa wakati wa uzinduzi, huduma ya gumzo ya AI inategemea Google Language Model for Dialogue Applications (LaMDA), ambayo ilizinduliwa miaka miwili iliyopita.

Jinsi gani Google Bard inafanya kazi?

LaMDA ilijengwa kwa kutumia Transformer, mfumo wa Google’s neural network architecture, ambao umetengenezwa a google na kuwa open source 2017, Kwa mujibu wa Google GPT-3 mfumo ambao unatumiwa na ChatGPT pia umetengeneza kwa kutumia Transformer.

Toleo la awali la Bard litatumia mfumo mwepesi wa LaMDA, kwa sababu inahitaji nguvu ndogo ya kompyuta na inaweza kupanuliwa kwa watumiaji zaidi, kulingana na taarifa. Bard itachukua data zote kutoka kwenye mtandao ili kutoa majibu sahihi. Pichai alisema kutumia habari kutoka kwenye wavuti kutatoa majibu “safi na yenye ubora wa hali ya juu.”

Kama ufahamu, ChatGPT inatumia data za mtandaoni ambazo zilichukuliwa hadi kufikia mwaka 2021, hii inafanya ChatGPT kuwa na ufahamu wa mambo mbalimbali hadi kufikia mwaka 2021. Kutokana na hilo ChatGPT haina uwezo wa kufahamu jambo lolote la kuanzia mwaka 2022 na kuendelea.

Nani Anaweza Kutumia Google Bard?

Google ilifungua orodha yake ya kusubiri (Waiting List) ya Bard mnamo Machi 21, 2023. Orodha ya kusubiri itatoa ufikiaji wa watumiaji wa nchini Marekani na Uingereza kwa awamu, Kwa sasa pia baadhi ya watumiaji wa nchi za Afrika wameanza kutumia mfumo wa Bard kwa majaribio.

Kwa sasa Google inakusanya maoni ya mapema kutoka kwa watumiaji ili kuendelea kuboresha mfumo huo wa Google Bard.

Jinsi ya Kuanza Kutumia Google Bard

Jinsi ya Kutumia Google Bard, Mfumo wa AI Kama ChatGPT

Kama unataka kutumia mfumo wa Google Bard unaweza kufanya hatua mbalimbali, Moja ya hatua unaweza kufanya ni kujiunga na orodha ya kusubiri kupitia link hapo chini.

Tembelea Tovuti Hapa

Baada ya kukubaliwa kujiunga na Google Bard utapata ujumbe kupitia barua pepe yako na moja kwa moja utaweza kuanza kutumia mfumo huu kutoka Google.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use