WhatsApp imekuwa na utaratibu wa kutoa list ya simu na mifumo ya uendeshaji ambayo haitofanya kazi sambamba na programu ya WhatsApp. Hadi sasa, WhatsApp inafanya kazi vizuri kwenye simu za Android zenye mfumo wa Android kuanzia Android 4.1 na kuendelea.
Kwa upande wa iOS mfumo huu unafanya kazi kwenye simu za iOs zenye mfumo kuanzia iOS 12 na kuendelea.Pia kwa mfumo wa KaiOS ni kuanzia KaiOS 2.5.0 na kuendelea.
Kwa mujibu wa Price in Tanzania, hivi karibuni watumiaji wa simu zifuatazo hawatoweza kuendelea kutumia programu za WhatsApp kwenye simu hizo ifikapo tarehe 31 mwezi wa 12.
Apple
- iPhone 5
- iPhone 5c
Samsung
- Galaxy Ace 2
- Galaxy Core
- Galaxy S2
- Galaxy S3 mini
- Galaxy Trend II
- Galaxy Trend Lite
- Galaxy Xcover 2
LG
- LG Enact
- Lucid 2
- Optimus 4X HD
- Optimus F3
- Optimus F3Q
- Optimus F5
- Optimus F6
- Optimus F7
- Optimus L2 II
- Optimus L3 II
- Optimus L3 II Dual
- Optimus L4 II
- Optimus L4 II Dual
- Optimus L5
- Optimus L5 Dual
- Optimus L5 II
- Optimus L7
- Optimus L7 II
- Optimus L7 II Dual
- Optimus Nitro HD
Sony
- Xperia Arc
- SXperia miro
- Xperia Neo L
Huawei
- Ascend D
- Ascend D1
- Ascend D2
- Ascend G740
- Ascend Mate
- Ascend P1
HTC
- HTC Desire 500
Kumbuka hii ni baadhi ya simu, list kamili itaendelea kuongezwa kadri muda unavyozidi kwenda. Pia ni muhimu kufahamu kuwa unaweza kuendelea kutumia WhatsApp kwenye simu hizi na nyingine ambazo zitatajwa kwa muda na baadae hutoweza kutumia kabisa.
Pia baadhi ya simu zitaweza kutumia matoleo ya zamani ya programu ya WhatsApp kama matoleo hayo hayakuzuiliwa kwa matumizi. Kwa mujibu wa WhatsApp, WhatsApp hutuma meseji moja kwa moja kwa watumiaji wa simu ambazo hazifanyi kazi sambamba na matoleo mapya ya programu hiyo.