Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Fahamu eSIM Mfumo Mpya wa Laini za Simu za Kidigitali

Fahamu aina mpya ya teknolojia ya laini za kidigitali
Fahamu eSIM Mfumo Mpya wa Laini za Simu za Kidigitali Fahamu eSIM Mfumo Mpya wa Laini za Simu za Kidigitali

Wakati dunia ikizidi kusonga mbela na teknolojia mpya za simu zinazojikunja na nyingine kama hizo, kampuni za mitandao ya simu nazo zimeanza kubadilika na kuja na teknolojia mpya za laini za simu za kidigitali au eSIM.

Kama wewe ni mmoja wa watu ambao wanapenda kujua zaidi kuhusu mfumo huu mpya wa laini za kidigitali basi unasoma makala sahihi, pia kama wewe ni mmoja wa watu ambao wanatarajia kununua matoleo mpya ya simu za iPhone, pamoja na iPad pia unasoma makala sahihi kwani simu hizi zote zinakuja na mfumo wa eSIM.

Advertisement

eSIM ni nini ?

Fahamu eSIM Mfumo Mpya wa Laini za Simu za Kidigitali

Kwa kirefu eSIM inamaana ya “embedded SIM card” hii ni aina mpya ya laini ya simu ambayo ili kutumia hauna haja ya kuwa na ile kadi ambayo unaweka kwenye simu yako, bali hii ni aina mpya ya laini ambayo ni ya kidigitali hivyo simu yako haina haja ya kuwa na sehemu ya kuweka laini ili kutumia huduma za kupiga na kupokea simu, kutuma SMS pamoja na kutumia Internet.

Ili kuwezesha huduma hii ya eSIM simu yako inatakiwa kuwa na chip maalum ambayo hii huwa ndani ya simu yako ambayo inauwezo wa kuunganisha huduma za kupiga simu na kutuma ujumbe mfupi bila kuwa na ile laini ya kawaida.

Chip hiyo hufanya kazi sawa na sehemu ile ya NFS ambayo iko kwenye simu nyingi za siku hizi. Kama unataka kujua zaidi kuhusu NFS unaweza kusoma makala hapa.

Je eSIM Inafanyaje Kazi ?

Kama nilivyo kueleza hapo juu, ili kusudi sehemu hii ya eSIM iweze kufanya kazi simu yako inatakiwa kuwa na teknolojia hiyo au Chip maalum ambayo inaweza kuuunganisha simu yako na mtandao wa simu bila kuweka laini ya kawaida.

Lakini pamoja na mahitaji hayo, pia kampuni zinazotoa huduma za simu zinatakiwa kuwa na aina mpya ya miundombinu ya kuwezesha kutoa huduma hizi kwani huduma hizi zina mahitaji ya miundo mbinu ya tofauti kabisa na huduma zile za kawaida.

Kwa mfano, endapo mteja anataka kuunganishwa na huduma hii ya eSIM inambidi aende kwa wakala au kwenye kampuni husika, kisha baada ya kufunguliwa akaunti atapewa mchoro wa QR Code ambao huu ndio utatumika kama laini ya simu. Sasa ili kuunganisha eSIM na simu yako mteja anatakiwa ku-scan QR code hizo na simu yake moja kwa moja itaunganishwa na mtandao husika.

Endapo mteja anataka kubadilisha laini ataenda kwa wakala wa kampuni husika kisha atapewa tena QR code za mtandao husika na ku-scan QR code hizo na hapo hapo mtandao utabadilika na kuwa mtandao alio uchagua. Kifupi ni kwamba code za QR Code ndizo zitakuwa za msingi kwani ndizo zitakazokuwa zinatumika kama kiunganishi cha simu yako na eSIM.

Je Huduma ya eSIM Ipo Tanzania ?

Kwa sasa huduma ya eSIM bado haijafika Tanzania, lakini kutokana na teknolojia hii kuendelea kutumika kwa wingi kwenye simu mbalimbali ikiwemo simu mpya za iPhone, pamoja na kuwepo kwa ushindani wa watoa huduma za simu hapa Tanzania pengine tegemea kusikia ujio teknolojia ya eSIM hivi karibuni.

Je kwa Sasa eSIM inatumika kwenye simu zipi ?

Kwa sasa kwa mujibu wa tovuti ya What Phone Plan, eSIM iapatika kwenye simu nyingi za nje ya nchi (ambazo haziwezi kutumika Tanzania) na kwa simu ambazo zinajulikana ndio kama hizo nilizo zitaja hapo juu yani iPhone XS, iPhone XR, na iPhone XS Max, pamoja na toleo jipya la iPad Pro.

Kuna Faida Gani na Hasara za Kutumia eSIM ?

Ukweli ni kwamba zipo faida nyingi sana za kutumia eSIM kwani itakuwa ni rahisi sana kwa mtumiaji kuwa na uwezo wa kutumia simu yake bila kubadilisha laini kila mara kwani eSIM inakuja na teknolojia ambayo unaweza kutumia kwenye eSIM kwenye nchi mbalimbali bila kubadilisha chochote.

Fahamu eSIM Mfumo Mpya wa Laini za Simu za Kidigitali

Moja ya hasara kubwa ya eSIM ni uwezo wa kiusalama, eSIM inatumia mfumo wa kidigitali zaidi hivyo hii hufanya data zako kuhifadhiwa na kampuni za simu na endapo kampuni za simu zikiduliwa basi ni rahisi sana wadukuzi kuchukua data zako. Vilevile kwa wale ambao wanapenda kuuza simu zilizotumika hii itabidi kuflash simu hizo kwanza ndipo ziweze kwenda kutumika na watu wengine kwani eSIM haitolewi kwenye simu.

Hitimisho

Natumaini hadi hapo utakuwa umepata angalau mwanga kidogo kuhusu eSIM. Kumbuka huko ndipo tunapokwenda hivyo ni lazima kwa wewe kuweza kuelewa kuhusu teknolojia hizi. Kwa sasa nadhani umeanza kuona matumizi ya QR code yamekuwa makubwa nadhani hii ni moja kati ya hatua za awali sana za kuleta teknolojia mpya kama hizi.

Kama una swali maoni au ushauri unaweza kuandika kupitia sehemu ya maoni hapo chini pia kwa habari zaidi za teknolojia hakikisha unatembelea tovuti ya Tanzania Tech kila siku.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use