Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Washa Tochi ya Smartphone kwa Kutingisha Simu

Washa tochi kwenye smartphone yako kwa haraka zaidi
Washa Tochi ya Smartphone kwa Kutingisha Simu Washa Tochi ya Smartphone kwa Kutingisha Simu

Najua ni wazi kuwa kila mtu ameshawahi kutembelea kwenye giza, iwe wewe ni mfanyakazi na umechelewa sana kurudi nyumbani au umetoka kwenye miangaiko yako na mvua imenyesha na kuna giza, basi hapo ndipo unapokuja umuhimu wa makala hii.

Leo nitaenda kuongelea njia mpya fupi na rahisi ya kuweza kuwasha tochi kwenye smartphone yako kwa haraka kwa kutingisha tu simu yako. Njia hii ni bora sana hasa kunapo kuwa na hali ya mvua na kuna giza na unajua mtaani kuna vidimbwi vya hapa na pale njia hii itakusaidia sana kwani huna haja ya kutoa simu yako na kuanza kutafuta sehemu ya kuwasha tochi kwani sasa utakuwa unatingisha tu simu yako na utaweza kuzima na kuwasha tochi kwa haraka.

Advertisement

Washa Tochi ya Smartphone kwa Kutingisha Simu

Kwa kuanza ni vyema ufahamu kuwa njia hii ni kwa ajili ya watumiaji wa simu za Android hivyo kama unatumia simu za iPhone njia hii haitofanya kazi kwenye simu yako. Basi baada ya kusema hayo moja kwa moja twende tujifunze maujanja haya.

Hatua ya kwanza unatakiwa kuingia kwenye soko la Play Store kisha download app inayoitwa Shake Flashlight & Camera, unaweza kupakua app hiyo kwa kutumia link hiyo hapo chini. Baada ya kupakua hakikisha una install vizuri kisha endelea kwenye hatua zifuatazo.

Download App Hapa

Fungua app hiyo kisha ipe ruhusa za muhimu ili iweze kuwasha tochi kwenye simu yako, kumbuka pia unaweza kuwasha kamera ya simu yako kwa kutumia njia kama hii ya kutingisha simu yako, hivyo usishangae pale app hii inapo omba ruhusa ya kuwasha kamera yako.

Washa Tochi ya Smartphone kwa Kutingisha Simu

Baada ya hapo sasa utaletwa kwenye ukurasa mkuu ambapo hapa ndipo utakapo tumia kuwasha app hii ili iweze kufanya kazi. Kwa upande wa kulia juu utaona kitufe chekundi kilichopo kama switch, bofya hapa kuweza kuwasha app hiyo.

Washa Tochi ya Smartphone kwa Kutingisha Simu

Baada ya hapo sasa utakuwa imekamilisha hatua zote, sasa tingisha simu yako mara mbili na utaweza kuona simu yako imewaka tochi na ukitingisha kwa mara ya pili utaweza kuona tochi kwenye simu yako imejizima yenyewe. Uzuri wa njia hii ni kuwa, baada ya kuwasha app hii mara ya kwanza huna haja tena ya kuwasha kioo cha simu yako ndipo tochi iweze kuwaka kitu cha muhimu ni kutingisha simu yako mara mbili na hapo hapo tochi itawaka huna haja ya kuwasha kioo cha simu yako

Mpaka hapo najua utakuwa umeweza kuwasha tochi ya simu yako kwa kutingisha simu yako, kama njia hii itakuwa imekusaidia basi tuambie kupitia sehemu ya maoni hapo chini. Kwa maujanja zaidi unaweza kusoma hapa kujua jinsi ya kutafsiri maandishi yoyote kwa kutumia kamera ya smartphone yako.

Kwa habari zaidi za teknolojia hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania Tech kila simu, pia kama unataka kujifunza maujanja kwa vitendo nakushauri uangalie channel yetu hapa, na kama ikikupendeza basi hakikisha una subscribe ili kujifunza zaidi pale tutakapo weka video mpya.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use