Fahamu Mabadiliko Yote ya Muhimu Mfumo wa iOS 16

Mfumo wa iOS 16 unategemewa kupatikana rasmi kuanzia Mwezi Julai
Fahamu Mabadiliko Yote ya Muhimu Mfumo wa iOS 16 Fahamu Mabadiliko Yote ya Muhimu Mfumo wa iOS 16

Hivi karibuni kampuni ya Apple kupitia mkutano wake wa WWDC 2022 imetangaza rasmi ujio wa mifumo yake mipya ya uendeshaji ikiwa pamoja na mfumo mpya wa iOS 16.

Kama wewe ni mmoja wa watumiaji wa simu za iPhone basi nadhani sasa ni wakati mzuri wa kufahamu kuhusu mfumo mpya wa iOS 16. Mfumo huu mpya unategemewa kufikia watumiaji wa simu za iPhone kuanzia iPhone 8 hadi iPhone 13.

Advertisement

Yapo mambo mengi sana ambayo unatakiwa kujua kuhusu mfumo wa iOS 16, lakini kupitia makala hii nakuahidi utaweza kufahamu yote ya muhimu kuhusu iOS 16 ikiwa pamoja na yale ambayo pengine utegemee kuona kwenye simu yako ya iPhone hivi karibuni.

Mabadiliko Muhimu ya iOS 16

Fahamu Mabadiliko Yote ya Muhimu Mfumo wa iOS 16

Kitu cha muhimu sana kwenye mfumo huu mpya wa iOS 16 ni pamoja na sehemu ya Lock screen ambayo sasa unaweza kufanya mabadiliko muhimu kama kuweka widget pamoja na njia mpya ya kuweka wallpaper pamoja na kusoma Notification.

Fahamu Mabadiliko Yote ya Muhimu Mfumo wa iOS 16

Mbali na hayo yapo mambo mengine mengi ya muhimu kufahamu kuhusu mfumo mpya wa iOS 16, hivyo basi bila kuendelea kupoteza muda wako zaidi bofya Play hapo chini kujua mabadiliko yote ya muhimu yanayo tarajiwa kuja kwenye iOS 16.

Kama umeangalia video yote hapo juu, basi hayo ndio mabadiliko ya muhimu kwenye mfumo wa iOS 16, mfumo ambao unategemewa kuja hivi karibuni kwenye simu yako ya iPhone.

Mbali na hayo unaweza kuangalia list hapo chini ili kujua kama simu yako ipo kwenye simu ambazo zitapokea mfumo huo hapo tarehe 20 mwezi huu.

Simu za iPhone Zitakazo Pokea iOS 16

Fahamu Mabadiliko Yote ya Muhimu Mfumo wa iOS 16

Kwa mujibu wa kampuni ya Apple, zifuatazo ndio simu zote za Apple ambazo zitapokea mfumo mpya wa iOS 16 hivi karibuni.

Fahamu Mabadiliko Yote ya Muhimu Mfumo wa iOS 16

  • iPhone 13
  • ‌iPhone 13‌ mini
  • iPhone 13 Pro
  • ‌iPhone 13 Pro‌ Max
  • iPhone 12
  • iPhone 12 mini
  • ‌iPhone 12‌ Pro
  • iPhone 12 Pro Max
  • iPhone 11
  • ‌iPhone 11‌ Pro
  • iPhone 11 Pro Max
  • ‌iPhone‌ XS
  • ‌iPhone‌ XS Max
  • ‌iPhone‌ XR
  • ‌iPhone‌ X
  • iPhone‌ 8
  • ‌iPhone‌ 8 Plus
  • ‌iPhone SE‌ (2nd generation or later)

Na hayo ndio yote ya muhimu ambayo unatakiwa kujua kuhusu mfumo mpya wa iOS 16, kama unataka kujua kuhusu mfumo wa iOS 15 basi unaweza kusoma hapa.

Kwa habari zaidi za teknolojia hakikisha unatembelea tovuti ya Tanzania Tech kila siku, pia usisahau kujiunga nasi kupitia channel yetu ya Tanzania Tech kupitia YouTube hapa.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use