Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Install Mfumo wa Windows 11 Bila PC Kuwa na TPM 2.0

Kama unataka kuinstall Windows 11 kwenye kompyuta isiyo na sifa soma makala hii
Install Mfumo wa Windows 11 Bila PC Kuwa na TPM 2.0 Install Mfumo wa Windows 11 Bila PC Kuwa na TPM 2.0

Hivi karibuni kampuni ya Microsoft inatarajia kuzindua rasmi kwa watumiaji mfumo mpya wa Windows 11, mfumo huu unatarajiwa kupatikana kama update kuanzia tarehe 5 mwezi huu oktoba kwa baadhi ya PC ambazo zimekidhi vigezo na masharti.

Lakini kama wewe ni mtumiaji wa Wndows na unataka kupakua mfumo mpya wa Windows 11 bila kompyuta yako kuwa na TPM 2.0 basi makala hii ni kwa ajili yako.

Advertisement

Kupitia makala hii nitakupa njia moja ambayo itaweza kusaidia sana kuweza kudownload toleo la Windows 11, pamoja na matoleo ya Windows 10 kama una hitaji. Kitu cha muhimu ni kufuata maelezo hapo chini na moja kwa moja utaweza kudownload na kuinstall Windows 11 bila kuwa na PC yenye uwezo wa TPM 2.0

Install Windows 11 bila PC kuwa na TPM 2.0

Kwa kuanza unatakiwa kudownload file ambalo litakusaidia kuweza kufanya hatua zote hizi, hakikisha unayo programu ya ZIP ili kuweza kufungua file hilo.

Install Mfumo wa Windows 11 Bila PC Kuwa na TPM 2.0

Download Programu Hapa

Baada ya kudownload, Unzip file husika kisha endelea kwenye hatua kama inavyo onekana kwenye video hapo chini.

Kama unavyoweza kuona, hatua hizi ni rahisi na huna haja ya kufanya kitu kingine zaidi ya kufungua file hili kisha bofya file la MediaCreationTool.bat, hakikisha kompyuta yako ime unganisha na Internet na una bando ya kutosha.

Baada ya hapo chagua toleo la Windows unalo hitaji kisha moja kwa moja utaweza kuchagua aina ya file unalo taka, kama ni ISO au aina nyingine za file ambazo utaweza kuinstall kwa urahisi zaidi.

Install Mfumo wa Windows 11 Bila PC Kuwa na TPM 2.0

Ukifuata hatua zote bila shaka utaweza kuinstall mfumo wa Windows 11 kwa urahisi kwenye kompyuta bila kuwa na sifa ya muhimu ambayo ni TPM 2.0

Kama unataka msaada zaidi unaweza kutuandikia kupitia kwenye maoni hapo chini, kwa maujanja zaidi kwa vitendo hakikisha una jiunga na channel yetu ya Tanzania Tech hapa ili kujifunza hatua hizi moja kwa moja kwa urahisi kwa lugha ya Kiswahili hakikisha hupitwi na makala hizi.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use