Baada ya habari kusambaa siku chache zilizopita kuhusu kampuni mama ya facebook kubadilisha jina, hatimaye hivi leo habari mpya zinasema kuwa kampuni ya Facebook sasa itakuwa inaitwa Meta.
Kwa mujibu wa ripoti hizo, Jina “Meta” ndio litakuwa jina la kampuni mama ambayo ina miliki apps za Facebook, Instagram, WhatsApp pamoja na kampuni ya Oculus.
Hata hivyo kwa mujibu wa Meta, kampuni hiyo sasa itakuwa inaendeshwa kwa pande mbili tofauti yaani upande wa software ambao utahusisha programu na apps zote unazo zijua na upande wa Reality Labs. Ambao utakuwa una husika na mambo yote ya teknolojia ya (VR) Virtual reality
na (AR) Augmented reality.
Mbali ya kuwa Facebook imebadilisha jina la kampuni mama kutoka Facebook kwenda Meta, bado hakuna kitu chochote kingine ambacho kimetangazwa kubadilika isipokuwa jina la kampuni hiyo ambayo sasa ndio itakuwa inajulikana kama mmiliki wa apps za Facebook, WhatsApp, na Instagram.
Unaweza kuangalia yote yaliyojiri kwenye uzinduzi wa Metaverse pamoja na jina jipya la kampuni hiyo ndani ya DK 10 kupitia video hapo chini.
.