Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Kampuni ya Facebook Kufikiria Kubadilisha Jina Lake

Facebook inatarajia kubadilisha jina la kampuni na sio jina la App
Kampuni ya Facebook Kufikiria Kubadilisha Jina Lake Kampuni ya Facebook Kufikiria Kubadilisha Jina Lake

Habari za hivi karibuni zinasema kuwa kampuni ya Facebook inafikiria kubadilisha jina lake la kampuni mapema mwezi huu.

Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vya habari, inasemekana kuwa facebook inatarajia kubadilisha jina hilo na kutengeneza jina jipya la kampuni ambalo ndio litakuwa jina mama la shughuli zote zinazo fanywa na kampuni ya Facebook.

Advertisement

Kwa sasa jina facebook linasimama kama jina la kampuni mama inayo miliki shughuli zote za kampuni ikiwa pamoja na umiliki wa app za Facebook, WhatsApp, Instagram pamoja na makampuni mengine yahusuyo teknolojia.

Hatua hizi zinakuja siku chache baada ya facebook kushutumiwa kuvunja sheria za mahali pakazi, pamoja na sheria nyingine za haki za binadamu.

Kwa sasa inasemekana kuwa mkurugenzi mtendaji wa Facebook Mark Zuckerberg, anatarajia kuwasilisha mapendekezo ya jina jipya kwenye mkutano wa ndani ambao utafanyika wiki ijayo.

Kumbuka kuwa Facebook haibadilishi jana la App yake, bali Facebook inatatajia kubadilisha jina la kampuni mama ambayo inamiliki app hizi na biashara nyingine. Hadi sasa kampuni inayo miliki app za Facebook, Instagram, WhatsApp na biashara nyingine bado inaitwa Facebook, Inc.

Mwaka 2015 kampuni ya Google nayo ilitangaza Alphabet kama jina la kampuni mama ya Google ambapo hii ili fanywa ili kukuza biashara na kuruhusu kampuni hiyo kufanya mambo mengi zaidi ya kile ambacho watu wengi ufahamu kuhusu Google kama search engine.

Kwa sasa bado hakuna taarifa juu ya jina jipya la kampuni hiyo, ila kwa mujibu wa taarifa mbalimbali inasemekana kuwa jina hilo litakuwa linahusisha neno “Horizon”.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use