Kama wewe ni mmoja wa watumiaji wa simu za Apple basi nadhani sasa ni wakati mzuri wa kufahamu kuhusu mfumo mpya wa iOS 15. Mfumo huu mpya unategemewa kutoka sambamba na simu mpya za iPhone 13 ambazo zimezunduliwa hivi karibuni.
Yapo mambo mengi sana ambayo unatakiwa kujua kuhusu mfumo wa iOS 15, lakini kupitia makala hii nakuahidi utaweza kufahamu yote ya muhimu kuhusu iOS 15 ikiwa pamoja na yale ambayo pengine utegemee kuona kwenye simu yako ya iPhone hivi karibuni.
Basi bila kuendelea kupoteza muda wako zaidi bofya Play hapo chini kujua mabadiliko yote ya muhimu yanayo tarajiwa kuja kwenye iOS 15.
Kama umeangalia video yote hapo juu, basi hayo ndio mabadiliko ya muhimu kwenye mfumo wa iOS 15, mfumo ambao unategemewa kuja na simu mpya za iPhone 13 tarehe 20 mwezi huu.
Mbali na hayo unaweza kuangalia list hapo chini ili kujua kama simu yako ipo kwenye simu ambazo zitapokea mfumo huo hapo tarehe 20 mwezi huu.
Simu za iPhone Zitakazo Pokea iOS 15
Kwa mujibu wa kampuni ya Apple, zifuatazo ndio simu zote za Apple ambazo zitapokea mfumo mpya wa iOS 15 hivi karibuni.
- iPhone 13
- iPhone 13 Mini
- iPhone 13 Pro
- iPhone 13 Pro Max
- iPhone 12
- iPhone 12 Mini
- iPhone 12 Pro
- iPhone 12 Pro Max
- iPhone 11
- iPhone 11 Pro
- iPhone 11 Pro Max
- iPhone XS
- iPhone XS Max
- iPhone XR
- iPhone X
- iPhone 8
- iPhone 8 Plus
- iPhone 7
- iPhone 7 Plus
- iPhone 6S
- iPhone 6S Plus
- iPhone SE (first and second generation)
- iPod Touch (seventh generation)
Na hayo ndio yote ya muhimu ambayo unatakiwa kujua kuhusu mfumo mpya wa iOS 15, kama unataka kujua kuhusu mfumo wa iOS 14 basi unaweza kusoma hapa.
Kwa habari zaidi za teknolojia hakikisha unatembelea tovuti ya Tanzania Tech kila siku, pia usisahau kujiunga nasi kupitia channel yetu ya Tanzania Tech kupitia YouTube hapa.