Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Biashara Unazoweza Kufanya Kupitia Mtandao wa Twitter

Biashara nzuri ambazo unaweza kufanya kupitia mtandao wa Twitter
Biashara Unazoweza Kufanya Kupitia Mtandao wa Twitter Biashara Unazoweza Kufanya Kupitia Mtandao wa Twitter
©clicktotweet.com

Twitter ni moja ya mtandao ambao unatumiwa na watu wengi sana ambao wanapenda kusoma, hivyo basi hii inafanya twitter kuwa mtandao bora sana kwa kufanya biashara za mtandaoni.

Kupitia makala hii nitaenda kushare na wewe aina 3 za biashara ambazo unaweza kufanya kupitia mtandao wa Twitter.

Advertisement

Biashara hizi zinaweza kufanywa na mtu yoyote ambae anayo akaunti ya twitter, na kama akaunti hiyo inayo wafuasi wa kutosha, lakini pia bila kusahau lazima uwe na jina kupitia mtandao huo.

Biashara Unazoweza Kufanya Kupitia Mtandao wa Twitter
©belvg.com

Kama unayo hayo yote basi bila kupoteza muda twende tuka angalie makala hii.

Uza Ujuzi Kupitia Twitter

Biashara Unazoweza Kufanya Kupitia Mtandao wa Twitter
©earnclax.com

Kama wewe ni mmoja wa watu ambao wana ujuzi fulani ambao unahitajika basi mahali bora kwa kuuza ujuzi wako ni kupitia Twitter.

Jinsi ya Kuanza

Unachotakiwa kufanya ni kutoa ushauri wa bure ambao unalingana na ujuzi ulio nao, kama unajua kuhusu biashara za mtandaoni basi unaweza kutoa ushauri wa bure kwa watu kuhusu biashara za mtandaoni.

Baada ya kutengeneza jina, unaweza kuanza kuhitaji gharama kuweza kutoa baadhi ya ujuzi ambao unaufahamu, pia unaweza kutengeneza kozi ambazo unaweza kuziuza moja kwa moja kupitia mtandao huo.

Niamini kuwa kama ushauri wako ni bora watu hawataona shida yoyote kulipia huduma yako. Kitu cha muhimu ni kutoa ushauri wa bure kwanza ili watu waone thamani ya huduma yako. Kamwe usiwe na haraka ya kupata mafanikio ya haraka kwani hii itakupa mafanikio ya mda mfupi tu!.

Anzisha Kurasa Zenye Kusaidia Jamii

Biashara Unazoweza Kufanya Kupitia Mtandao wa Twitter
©elimikawikiendi

Kupitia Twitter unaweza kuanzisha kurasa zenye kuelimisha, kurasa hizi zinaweza kuwa zimejikita kwenye mada moja au unaweza kujikita kwenye mada zote zinazogusa jamii.

Mfano wa kurasa kama hizi ni #ElimikaWikiendi, kurasa hii imejikita kutoa elimu kwa wote na unaweza kujiuliza mtu anawezaje kutengeneza pesa kupitia hii.

Jinsi ya Kuanza

Unatakiwa kuchagua mada ambayo unajua inagusa jamii kubwa ya watu, kisha tengeneza kurasa kupitia mtandao wa Twitter kisha anza kuchapisha tweet zenye kutoa elimu kupitia mada uliyo chagua.

Hakikisha mada unayo ichagua pia inagusa watu wa aina zote kwani hii itasaidia kufanya uweze kupata endorsement mbalimbali ambazo zinaweza kusaidia kukuza kurasa yako zaidi na pia kutengeneza pesa kupitia ukurasa wako.

Kitu cha muhimu ni kuwa kwenye aina hii ya biashara unatakiwa kuhakikisha kuwa unacho anzisha unakipenda kwa asilimia 100 na isiwe una anza kwaajili ya kupata pesa, hii ni kwa sababu siku zote “Pesa ni matokeo hivyo huja mwishoni”.

Uza Bidhaa za Kidigitali

Biashara Unazoweza Kufanya Kupitia Mtandao wa Twitter
©myva360.com

Twitter ni moja ya mitandao ambayo inaruhusu kuweka link, unaweza kutumia link kuuza bidhaa za kidigitali moja kwa moja kupitia mtandao wa Twitter.

Jinsi ya Kuanza

Tofauti na biashara nyingine kwenye list hii, biashara ya kuuza bidhaa za kidigitali inahitaji kuwa tayari umesha tengeneza brand, hivyo ni ngumu sana kuanza biashara hii mara moja.

Unahitaji kutengeneza brand kwanza kabla ya kuamua kufanya biashara hii, kwani moja kati ya kitu ambacho watu wengi hawapendi kupitia mtandao wa twitter ni LINK. Hii ni zaidi kama watumiaji hawa amini akaunti yako hivyo ni vizuri sana kutengeneza brand kwa kufanya moja ya biashara hapo juu kisha ndipo uje kwenye biashara hii ya kuuza bidhaa za kidigitali.

Hitimisho

Twitter ni moja ya mtandao ambao unatumiwa na watu wengi ambao wanapenda kusoma, hivyo hakikisha njia yoyote ya biashara unayo chagua ni vizuri kuwa na uwezo wa kutoa elimu kwa maneno machache.

Sio kila mtu anaweza kufanya hivi hivyo hakikisha unajifunza kutoa elimu kwanza kabla ya kufikiria kutengeneza pesa kupitia mtandao wa Twitter, ni muhimu kuwa na ratiba maalum ambayo pia itasaidia wafuasi wako kutokosa kitu chochote ambacho umeamua kufundisha au kutoa elimu.

Kwa kusema hayo moja kwa moja tumekamilisha makala hii, kama unalo jambo la kuongeza au kama una swali au maoni unaweza kuuliza kupitia sehemu ya maoni hapo chini. Kwa makala kama hizi hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania Tech kila siku. Pia unaweza kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech kupitia YouTube ili kujifunza zaidi kwa vitendo.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use