Unatumia Samsung.? Tumia Fingerprint Kufanya Hivi

Utaweza kufanya zaidi ya kufunga na kufungua simu yako
Unatumia Samsung.? Tumia Fingerprint Kufanya Hivi Unatumia Samsung.? Tumia Fingerprint Kufanya Hivi
©phandroid.com

Samsung ni simu ambazo zinatumiwa sana na watumiaji wa simu za Android, mbali ya kuwa ni simu zenye umri mkubwa zaidi kwenye soko lakini pia ni simu ambazo zinaongoza kwa kupokea update za mifumo mpya ya Android ambayo huwa inakuja na sehemu mpya mbalimbali.

Moja kati ya sehemu ambayo mimi binafsi nimekuwa nikitumia kwa muda mrefu ni sehemu ya Fingerprint. Binafsi sehemu hii nimekuwa niki itumia zaidi ya sehemu ya ulinzi ya kufunga na kufungua simu yangu.

Advertisement

Kupitia makala hii nitaenda kushare na wewe njia ambayo kwa namna moja ama nyingine itaweza kusaidia kuweza kutumia sehemu hii kwenye simu yako kwa namna ya tofauti na kuweza kurahisha matumizi yako ya simu ya Samsung.

Kitu cha muhimu hakikisha unafuata maelezo yote ili kuweza kufurahia sehemu hii.

Mahitaji Muhimu

Kabla ya kuanza kutumia sehemu ya Fingerprint kwa namna ya tofauti kitu cha muhimu ni kuhakikisha kuwa simu yako ni Samsung, pia hakikisha kuwa simu yako ina mfumo mpya wa Android 10 au Android 11. Pia ni vizuri zaidi kama simu yako itakuwa na sehemu ya Fingerprint kwa nyuma hii italeta maana zaidi kutumia sehemu hii kuliko sehemu hii ikiwa kwa mbele.

Tumia Fingerprint Kundesha Simu ya Samsung

Sasa kupitia sehemu ya fingerprint ya simu yako ya Samsung utaweza kuendesha simu yako kwa kufungua sehemu ya notification iliyopo juu ya simu yako bila kushika kioo cha simu yako. Utakachofanya ni kuslide kidole kwa kwenda chini kwenye sehemu ya fingerprint na utaona sehemu ya notification imefunguka na pia ukirudisha juu utaweza kufungua sehemu hiyo.

Hii ni muhimu sana hasa ukiwa unatumia simu yako kwa mkono mmoja, wote tunajua kuwa Notification ni sehemu inayo tumiwa zaidi kuliko sehemu nyingine na ili kufungua sehemu ya notification iliyopo juu ya simu yako ni lazima kushika simu yako kwa mikono miwili

Unatumia Samsung.? Tumia Fingerprint Kufanya Hivi

Sehemu hii inakusaidia kupunguza hii kwa kufungukua sehemu ya hiyo kwa haraka bila kushika kioo cha simu yako kwa haraka kabisa.

Jinsi ya Kuwasha Sehemu Hii Kwenye Samsung

Kama unatumia simu ya Samsung yenye mfumo wa Android 10 au Android 11 moja kwa moja unaweza kuwasha sehemu hii kupitia simu yako. Unachotakiwa kufanya ni kufungua sehemu ya Settings kisha bofya Advanced Features.

Unatumia Samsung.? Tumia Fingerprint Kufanya Hivi

Kisha baada ya hapo utafunguka ukurasa mwingine na chagua sehemu ya Motion and gestures ambayo ni sehemu ya nne kutoka juu.

Unatumia Samsung.? Tumia Fingerprint Kufanya Hivi

Baada ya hapo moja kwa moja unachotakiwa kufanya ni kuchagua kwa kuwasha sehemu ya Fingerprint gesture ambayo ipo chini kabisa wa ukurasa huo. Hakikisha sehemu hii imewashwa kwa kuwa na alama ya Blue kama inavyo onekana kwenye picha hapo chini.

Unatumia Samsung.? Tumia Fingerprint Kufanya Hivi

Baada ya hapo moja kwa moja utakuwa umewasha sehemu hiyo na sasa unaweza kutumia sehemu ya fingerprint kufungua sehemu ya notification bila kushika kioo cha simu yako.

Kama simu yako inayo fingerprint kwa nyuma utaweza kufurahia zaidi sehemu hii kwa kuwa unaweza kushika simu yako kwa mkono mmoja ikiwa pamoja na kupapasa sehemu ya fingerprint kwa urahisi zaidi kuliko simu ambayo inayo fingerprint kwa mbele.

Bila shaka sehemu hii inaweza kuwa imekusaidia kwa namna moja ama nyingine, kama unataka kujifunza zaidi hakisha unatembelea channel yetu ya Tanzania tech hapa. Kama unataka kujifunza zaidi kuhusu fingerprint unweza kusoma hapa jinsi ya kuweka ulinzi wa fingerprint kwenye app yoyote kwenye simu yako ya Android.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use