Hivi karibuni tuiongelea kuhusu sifa za muhimu za kuangalia kabla ya kununua laptop, na moja kati ya jambo la muhimu ambalo tuliangalia ilikuwa ni processor.
Sasa najua kuwa wengi wenu mnajua kuhusu processor hivyo sitopoteza muda mwingi kueleza kuhusu processor ni nini hivyo moja kwa moja nitaenda kwenye makala ya leo ambayo naamini itakusaidia sana kuweza kujua processor za laptop kwa umakini zaidi.
TABLE OF CONTENTS
Fahamu Herufi “Y-U-H” kwenye Laptop
Kama ulivyoweza kusoma kicha hapo juu, leo nitaenda kukujuza maujanja ambayo inawezekana ulikuwa hujui kuhusu laptop. Maujanja haya yatakusaidia sana pale unapotaka kununua laptop hasa hapa nchini Tanzania.
Ukweli ni kwamba nguvu ya laptop ipo kwenye processor, hata kama laptop ina RAM kubwa kiasi gani, au Hard Disk au SSD kubwa kiasi gani, kama laptop haina processor bora ni wazi kuwa bado itashindwa kufanya kazi vizuri.
Sasa katika swala zima la uwezo wa processor hapa ndipo herufi hizi “Y-U-H” zinapokuja kwenye matumizi.
Herufi kwenye Processor
Kama unataka kununua laptop na umeingia kwenye tovuti husika na kuangalia aina ya proceesor unaweza kukuta sifa ya processor imeandikwa hivi, Intel Core i7-8700K.
Sasa kwa mfano kwenye sifa hizi Intel Core i7-8700K unaweza kuona herufi ya mwisho kwenye processor hii ni U, yaani Intel Core i7-8700K.
Sasa herufi hii ndio inayo onyesha aina ya laptop na unayotaka kununua pamoja na uwezo wake wa processor.
Herufi “Y” Kwenye Processor za Laptop
Ukikutana na laptop yenye processor yenye herufi Y mwisho wa processor hii ina maana hizi ni zile laptop ambazo zina muundo kama tablet na mara nyingi laptop hizi zinakuja zikiwa hazina feni wala hazina vitu vingi ambayo vipo kwenye laptop nyingi za kawaida. Pia uwezo wa laptop hizi huwa ni mdogo kulinganisha na laptop nyingine.
Herufi “U” Kwenye Processor za Laptop
Ukikutana na laptop yenye processor yenye herufi U mwisho wa processor hii ina maana kuwa laptop hii ni nyembamba na mara nyingi laptop hizi huwa na kioo cha kati ya inch 13 na inch 14.
Pia huwa ni laptop zenye nguvu kiasi. Processor za laptop zenye herufi hii huwa kati ya Core i3, Core i5 na Core i7.
Herufi “H” Kwenye Processor za Laptop
Ukikutana na laptop yenye processor yenye herufi H mwisho wa processor hii ina maana kuwa laptop hii imetengeneza kwa kazi zaidi na hivyo laptop hizi mara nyingi huwa na processor kubwa na yenye nguvu.
Pia laptop hizi huwa kati ya inch 15 hadi inch 17. Processor za laptop zenye herufi hii huwa kati ya Core i5, Core i7 na Core i9.
Herufi “K” Kwenye Processor za Laptop
Ukikutana na laptop yenye processor yenye herufi K mwisho wa processor hii ina maanisha processor hizi zina nguvu zaidi na pia huwa unlocked na huweza kuongezwa uwezo au clock speed na mtumiaji wa kawaida, mara nyingi processor zenye herufi hii huwa zenye nguvu na hutumika mara nyingi kwenye Workstation.
Herufi “G” Kwenye Processor za Laptop
Ukikutana na laptop yenye processor yenye herufi G mwisho wa processor hii ina maana kuwa laptop hii inakuja na graphics ambayo imetengenzwa ndani ya chip hivyo laptop hizi ni za kawaida kwa matumizi ya kawaida.
Hitimisho
Kwa kusema hayo zipo herufi nyingi kwenye processor za intel, lakini kwa laptop ni muhimu kuangalia herufi hizi tatu “Y-U-H”.
Kitu cha muhimu pia ni kuwa zipo laptop ambazo hazina herufi zozote na kwa mujibu wa tovuti ya Intel hizo huwa na uwezo wa kawaida kulinganisha na nyingine.
Kama unataka kuona list nzima na maana yake unaweza kusoma hapa kila maana ya processor na maana yake ikiwa pamoja na processor za desktop.
Kama unataka kujifunza zaidi unaweza kutembelea channel yetu ya YouTube hapa, kwa maujanja zaidi kuhusu kompyuta hakikisha unapitia kipengele cha laptop na kompyuta hapa.