Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Jinsi ya Kupata iPhone Iliyopotea Hata Kama Imezima

Utaweza kupata iPhone yako hata kama imefutwa kila kitu au imefanyiwa Factory reset
Jinsi ya Kupata iPhone Iliyopotea Hata Kama Imezima Jinsi ya Kupata iPhone Iliyopotea Hata Kama Imezima
©imobie-resource.com

iPhone ni moja kati ya simu ambazo hutumiwa na watu wengi ambao hawapendi mambo mengi, hii ni kutokana na uhaba wa kufanya mambo mengi ambayo simu za Android zinaweza kufanya.

Lakini moja kati ya kitu ambacho simu za iPhone zinatazamiwa kufanya vizuri kuliko simu za Android ni kwenye swala zima la ulinzi. Kwa sasa naweza kusema kati ya Android na iPhone ni wazi kuwa iPhone ni simu bora sana hasa linapokuja swala zima la Ulinzi.

Advertisement

Kuliona hili leo nimekuletea makala ambayo itakusaidia kuweza kufanya jambo ambalo litakusaidia sana kulinda simu yako pale inapo potea au kuibiwa.

Kupitia makala hii nitakuonyesha jinsi ya kupata simu yako ya iPhone iliyopotea au iliyo ibiwa hata kama imezima au hata kama imefutwa kila kitu au Factory reset.

Jinsi Sehemu Hii Inavyofanya Kazi

Kabla ya kuendelea kwenye hatua za jinsi ya kupata simu yako ya iPhone iliyopotea ni vizuri kwanza kukwambia kuhusu sehemu hiyo ikiwa pamoja na simu gani za iPhone zenye uwezo wa kutumia sehemu hii.

Kwa kuanza kwanza ni vyema kufahamu kuwa sehemu hii ni mpya na inapatikana kwenye mfumo wa iOS 15 na kuendelea.

Jinsi sehemu hiyo inavyofanya kazi ni kuwa, kwa mujibu wa Apple pale unapozima simu yako ya iPhone basi ni vizuri kujua kuwa simu yako haizimi kabisa bali simu yako inakuwa kwenye hali ya kupunguza nguvu au “low-power state”.

Hii husaidia baadhi ya vitu kuendelea kufanya kazi kama kawaida ikiwa pamoja na sehemu ya “Find My Network” ambayo huweza kutuma data za simu yako ilipo hata kama simu imezima au imefutwa kila kitu.

Pale simu yako ya iPhone inapo pungua chaji na kufikia hatua ya kuzima, na kama umesha update kwenye mfumo wa iOS 15 na kuendelea utaona ujumbe kama huo kwenye picha hapo chini ukieleza kuwa simu yako itaendelea kuonekana kwenye Find My hata kama simu imezima au imefutwa.

Jinsi ya Kupata iPhone Iliyopotea Hata Kama Imezima

Ujumbe huu unaonyesha wazi kuwa sasa Apple wameleta sehemu hii ambayo itakusaidia kupata simu yako ya iPhone hata kama imezima au imefutwa kila kitu.

iPhone Zenye Uwezo Kupatikana Hata Kama Zimezimwa

Sasa kama nilivyo kwambia hapo juu, uwezo wa kupata simu yako ya iPhone inapo potea hata kama imezima au kufutwa kila kitu unapatikana kwenye simu za iPhone zenye mfumo wa iOS 15.

Lakini pia sio kila simu yenye uwezo huo na kwa mujibu wa Apple kwa sasa simu kwenye list hapo chini ndizo zenye uwezo wa kupatikana hata kama zimezima au hata kama mtu amefuta kila kitu.

Kumbuka list hii inaweza kuja kuongezeka hapo baadae baada ya Apple kuzindua matoleo mapya ya iphone hivi karibuni.

Jinsi ya Kuwasha Sehemu Hii

Baada ya kufahamu kidogo kuhusu sehemu hii sasa moja kwa moja twende kwenye hatua jinsi ya kuwasha sehemu hii kupitia simu yako ya iPhone yenye mfumo wa iOS 15. Kabla ya yote hakikisha sehemu ya Find My iPhone na Find My network zimewashwa kwenye simu yako.

Kwa kuanza Fungua Sehemu ya Settings kwenye simu yako ya iPhone.

Jinsi ya Kupata iPhone Iliyopotea Hata Kama Imezima

Baada ya hapo bofya sehemu ya Profile yako ipo juu kabisa baada ya kufungua sehemu ya Settings.

Jinsi ya Kupata iPhone Iliyopotea Hata Kama Imezima

Baada ya hapo tafuta sehemu ya Find My, kisha fungua sehemu hiyo na hakikisha sehemu ya Find My iPhone ipo On au imewashwa.

Jinsi ya Kupata iPhone Iliyopotea Hata Kama Imezima

Pia hakikisha sehemu ya Find My network pia imewashwa kwenye simu yako ya iPhone kama invyo onekana kwenye picha hapo chini. Hivyo kwa ufupi hakikisha sehemu ya Find My iPhone na Find My network zote zikiwa zimewashwa pamoja na Sehemu ya Send last location.

Jinsi ya Kupata iPhone Iliyopotea Hata Kama Imezima

Baada ya kuwasha sehemu hii moja kwa moja simu yako itakuwa inaweza kupatikana hata kama imezimwa au hata kama imeibiwa na kufutwa kila kitu. Moja kwa moja twende tukangalie njia za kupata simu yako ya iPhone iliyo ibiwa au kupotea.

Kupata Simu ya iPhone iliyozima au Kufutwa Kila Kitu

Hatua ya kwanza kama unayo simu nyingine ya iPhone moja kwa moja nenda kwenye app ya Find My. Kisha bofya sehemu ya “Devices”.

Jinsi ya Kupata iPhone Iliyopotea Hata Kama Imezima

Baada ya hapo chagua simu ya iPhone ambayo unataka kuona mahali ilipo na moja kwa moja kupitia app hiyo utaweza kuona ramani mahali simu yako ilipo.

Kwa Kutumia iPhone ya Mtu Mwingine

Kama huna simu ya iPhone au kifaa chochote cha Apple, unaweza kutumia simu ya mtu mwingine moja kwa moja kupata simu yako ya iPhone iliyozima au kufutwa kila kitu.

Fungua App ya Find My kwenye simu ya mtu, kisha moja kwa moja bofya sehemu ya Me ambayo ipo chini upande wa kulia.

Jinsi ya Kupata iPhone Iliyopotea Hata Kama Imezima

Baada ya kubofya hapo shuka mpaka mwisho kabisa wa ukurasa huu, kisha endelea kwa kubofya sehemu ya “Help a Friend”, baada ya hapo unatakiwa kuingia kwenye akaunti yako ya iCloud ambayo inatumika kwenye simu iliyozima au kufutwa kabisa.

Jinsi ya Kupata iPhone Iliyopotea Hata Kama Imezima

Baada ya hapo moja kwa moja chagua simu ya iPhone ambayo unataka kupata au kujua mahali ilipo na moja kwa moja utaweza kuona simu yako kwenye ramani hata kama imezima au hata kama imefutwa kila kitu au hata kama imefanyiwa Factory reset.

Kwa kutumia Website ya iCloud

Pia kama huna iphone nyingine, na pia huna rafiki ambaye anayo simu ya iPhone basi moja kwa moja unaweza kutumia tovuti ya iCloud kupitia kifaa chochote chenye uwezo wa kutumia browser na internet.

  • Kwa kuanza tembelea tovuti ya iCloud.com
  • Kisha moja kwa moja ingia kwenye akaunti yako kwa kutumia akaunti yako ya iCloud inayotumika kwenye simu iliyopotea kisha bofya “Find iPhone“.

Jinsi ya Kupata iPhone Iliyopotea Hata Kama Imezima

Unaweza kuuliza password kwa mara ya pili kisha baada ya kujaza password yako moja kwa moja utaweza kupata ramani yenye kuonyesha mahali simu yako ilipo.

Hitimisho

Na hiyo ndio njia ambayo unaweza kutumia kupata simu yako ya iPhone iliyopotea au kuibiwa hata kama imezima au imefutwa kila kitu. Ni wazi njia hii itasaidia sana kupunguza wizi wa simu mpya za iPhone hivyo ni wazi kuwa simu za iPhone zinaendelea kuwa kinara kwenye swala zima la ulinzi.

Kama unataka kujifunza zaidi unaweza kusoma hapa kujua baadhi ya njia ambazo unaweza kuongeza ulinzi kwenye simu yako ya Android. Kwa maujanja zaidi hakikisha una tembelea channel yetu ya YouTube Hapa, nakuahakidi hutojutia..!

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use