Ni wazi kuwa umeshakutana na ushauri mwingi sana unapotaka kununua laptop, lakini ukweli ni kwamba kila mtu ana pendekezo lake hasa kulingana na kazi au hitaji lake ikiwa pamoja na uwezo wa kumudu bei.
Sasa kuliona hili leo nimeona nikuletee makala ya tofauti ambayo naamini haita kuchosha ambayo itakusaidia sana kuweza kupata laptop bora na ambayo itadumu kwa muda mrefu.
Tofauti na makala nyingine ambazo umewahi kusoma, makala hii ina angazia zaidi kwenye sifa ambazo unahitaji kwenye laptop yako, iwe laptop kwa ajili ya kazi au laptop ya matumizi mengine. Bila kuendelea kupoteza muda wako zaidi moja kwa moja kwenye makala hii
TABLE OF CONTENTS
Sifa za Kuangalia Unapo Nunua Laptop
Kwa kuanza kama hutaki kusoma maelezo ya muhimu na kama huna muda mwingi unaweza kuishia hapa (kwenye picha) kwa kusoma sifa hizi ambazo unahitaji kwenye laptop yako.
Hakikisha laptop unayotaka kununua inakuja na sifa zifuatazo au zaidi ya hapa lakini ni muhimu kuhakikisha sio chini ya hapa.
Processor
Hakikisha Laptop ina Processor ya Intel Core i7, Intel Core i9 au AMD Ryzen 5 / 7 au zaidi ya hapa. Hakikisha haununui laptop yoyote yenye processor ya intel Pentium na Intel Celeron maana hizi zinakua na uwezo mdogo sana na pia kwa sasa programu nyingi hazikubali kwenye laptop zenye processor hizi
RAM
Hakikisha laptop unayotaka kununua inakuja na RAM isiyo pungua GB 8 na kuendelea, hii ni muhimu kwani ukubwa wa RAM ufananishwa na uwezo wa processor hivyo laptop zenye uwezo mkubwa wa RAM huwa na uwezo mkubwa wa Processor. Unaweza kuongeza RAM baaae lakini ni muhimu kuangalia RAM inayokuja na laptop kwanza.
Uhifadhi wa Ndani
Kama unataka kununua laptop yenye uwezo mzuri wa kudumu kwa muda mrefu bila kufikiria hasara ya kupoteza vitu vyako baadae, basi ni muhimu kununua laptop yenye mfumo wa uhifadhi wa SSD na sio HDD. Unaweza kusoma tofauti ya HDD na SSD hapo chini, lakini ni muhimu kujua kuwa SSD inauwezo mkubwa wa kufanya kazi kwa haraka na kudumu zaidi kwa muda mrefu kuliko HDD.
Ports / Viunganishi
Kwa kuwa hapa kwetu Tanzania bado baadhi ya vitu vipo slow, ni wazi kuwa HDMI kwa sasa ndio moja kati ya port ambayo ni muhimu sana. Hii itakusaidia kuunganisha vitu kama TV au Monitor nyingine na hii ni muhimu sana. Lakini kama unaweza ni vizuri kuangalia laptop yenye USB-C au Thunder bolt hii itakusaidia sana hapo baadae kwani huko ndipo tunapo kwenda.
Graphics
Kama unataka laptop kwa ajili ya kazi za kuedit picha na video basi ni muhimu kuzingatia zaidi processor na Graphics. Kwa upande wa Graphics ni vyema kuangalia laptop yenye dedicated graphics card, unaweza kuangalia graphics za MX 250, GTX 1650 au RTX 2060 au zaidi. Kama kazi zako ni za kawaida graphics sio ya muhimu sana.
Battery
Nimeacha battery ya mwisho kabisa kutokana na kuwa huwezi kujua kiwango halisi cha battery mpaka utumie laptop husika. Kuna tofauti kati ya kiwango cha kudumu battery kinacho andikwa kwenye sifa na kiwango ambacho utakipata wakati unatumia laptop husika. Hii ni kutokana na kuwa matumizi hutofautiana. Hivyo basi ni muhimu kuwa na laptop yenye battery kubwa lakini hii haina maana kuwa itadumu na chaji kwa muda mrefu zaidi.
Hitimisho
Kifupi kabisa ni vizuri kufahamu kununua laptop kunatokana na bajeti ya mtu aliyo nayo, ikiwa pamoja na aina ya kazi ambayo anataka laptop hiyo ifanye hivyo ni muhimu sana kuzingatia hayo kabla ya kununua laptop unayo hitaji.
Kitu kingine kuna picha hapo juu yenye herufi Y – U – H, kama unataka kujua nini maana ya herufi hizo na kwanini ni muhimu kufahamu unapotaka kununua laptop basi unaweza kusoma hapa makala yenye kuelezea kwanini ni muhimu kuangalia herufi hizo unapotaka kununua laptop kwaajili ya kazi yoyote..
Kama unataka kujifunza zaidi hakiksha una Subscribe kwenye channel yetu ya YouTube hapa.