Kwa muda sasa nimekua nikipokea maombi ya kufundisha watu mbalimbali jinsi ya kutengeneza programu na website mbalimbali. Kwa kuwa muda hautoshi inanibidi kutoa masomo hapa hasa kwenye hatua za kutengeneza website ambazo zinaweza kusaidia kutengeneza pesa mtandaoni.
Lakini kama wewe ni mmoja wa watu ambao wanataka kujifunza kutengeneza website au application mbalimbali basi makala hii ni kwaajili yako. Kupitia makala hii utaweza kufahamu tovuti ambazo zinaweza kusaidia kujifunza bure kabisa hatua za kutengeneza website au apps.
Kama ilivyo kawaida ya kujifunza, ni muhimu kujua kuwa hatua ya kujifunza huchukua muda na ni muhimu kuwa na malengo ya muda mrefu kuliko kufikiria zaidi kutengeneza programu fulani. Kupitia tovuti hizi utaweza kujifunza lugha mbalimbali za kompyuta ambazo ni muhimu kama unataka kujifunza kutengeneza programu yoyote au website.
Baada ya kusema hayo, moja kwa moja twende kwenye tovuti hizi ambazo zinaweza kusaidia wewe kujifunza kutengeneza programu au tovuti mbalimbali.
TABLE OF CONTENTS
Sololearn
Solo learn ni moja kati ya tovuti ambazo binafsi nazitumia hadi leo kujifunza kuhusu python, java na lugha zingine za kutengeneza programu. Ukweli ni kwamba tovuti hii ni bora sana na inakupa somo kamili mwanzo hadi mwisho kwa maandishi pamoja na kwa kutumia video.
Kizuri zaidi kuhusu tovuti hii ni kuwa unasoma masomo yote haya bure kabisa bila kulipia kitu chochote. Kama ukizingatia mafunzo ya tovuti hii basi huna haja ya kujua tovuti nyingine. Tovuti hii pia inayo app za Android na iOS na unaweza kupakua app hizo hapo chini.
Khanacademy
Khan academy ni tovuti nyingine ambayo unaweza kutumia kujifunza kutengeneza apps na website mbalimbali. Mbali ya hayo, kupitia tovuti hii utaweza kujifunza mambo mengine mbalimbali ambayo ni tofauti na kompyuta. Utaweza kujifunza kozi mbalimbali za darasani ambazo ni muhimu kwa wanafunzi mbalimbali.
Tovuti ya Khan academy hii pia inayo app za Android na iOS na unaweza kupakua app hizo hapo chini.
Coursera
Kama wewe ni mtumiaji wa kompyuta wa muda mrefu basi ni wazi lazima kwa namna moja ama nyingine umeshawahi kusikia kuhusu tovuti hii. Tovuti hii ni moja kati ya tovuti bora sana za kujifunza kutengeneza programu na website na mambo mengine yahusuyo kompyuta kwa ujumla.
Tovuti hii ni moja ya tovuti ambazo zilinisaidia kupata ajira miaka ya nyuma kutokana na kuwa na vyeti vingi vya kuhitimi kozi zao mbalimbali. Ukweli nakwambia kama wewe ni mtumiaji wa kompyuta au unataka kujifunza basi tovuti hii ni muhimu sana yani sana.
Bitdegree
Bit degree ni tovuti nyingine ambayo unaweza kutumia kujifunza kutengeneza programu mbalimbali pamoja na apps mbalimbali. Tovuti hii inakupa zaidi maelezo ya maandishi pamoja na video huku ikikupa mifano ambayo inaweza kusaidia zaidi kuelewa kwa haraka.
Mbali na hayo tovuti hii ni rahisi sana kutumia na ni moja kati ya tovuti ambazo unaweza kuanza kutumia kama hujui chochote kuhusu kompyuta, anza sasa kujifunza kupitia link hapo chini.
Na hizo ndio baadhi tu ya tovuti ambazo unaweza kuzitumia kujifunza kutengeneza apps na website mbalimbali. Kama unataka kujifunza zaidi unaweza kusoma hapa kujua channel za YouTube ambazo zinaweza kusaidia kujifunza kutengeneza apps na website.