Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Simu za Samsung Zitakazopata Mfumo wa One UI 4.0

List ya simu za Samsung zitakazo pata mfumo mpya wa Android 12
Simu za Samsung Zitakazopata Mfumo wa One UI 4.0 Simu za Samsung Zitakazopata Mfumo wa One UI 4.0

Kampuni ya Samsung inatarajia kuzindua mfumo wake mpya wa One UI 4.0 baadae mwaka huu, mfumo huo mpya unategemewa kuwa sambamba na mfumo wa Android 12 ambao ni mfumo wa maboresho wa Android 11.

Kwa sasa kampuni ya Samsung bado haija tangaza rasmi list ya simu zitakazo pokea mfumo mpya wa Android 12, lakini kwa mujibu wa ahadi ya samsung kuhusu idadi ya masasisho ambayo simu itakpokea, tumekuandalia list ya simu za Samsung Galaxy ambazo zitapokea One UI 4.0.

Advertisement

Hata hivyo kampuni ya Samsung imethibitisha kuwa inategemea kutoka mfumo wa One UI 3.5 mapema mwezi nane, huku toleo la One UI 4.0 likiwa ni toleo kubwa baada ya toleo la One UI 3.5. Hivyo basi simu ambazo zipo kwenye list hii ni simu ambazo zitapokea One UI 3.5, pamoja na toleo kuu la One UI 4.0 ambalo ndio litakuwa toleo kuu au Major Update kwa simu nyingi.

Hata hivyo simu nyingi za Samsung za miaka ya nyuma ambazo zitapokea One UI 4.0 zitakuwa zimepata toleo la mwisho kubwa na huenda simu nyingi za miaka ya nyuma  zisiendelee kupokea matoleo mengine makubwa. Simu ambazo zitakuwa za miaka ya karibuni zitaendelea kupokea matoleo makubwa ya One UI pamoa na Android mpya (Android 13) hapo baadae.

Simu za Samsung Galaxy Zitakazopata One UI 4.0

Kwa kusema hayo, hii hapa orodha ya vifaa vya Samsung Galaxy ambavyo vitapata sasisho la One UI 4.0, mara tu itakapoanza kutoka baadaye mwaka huu.

Samsung Galaxy S Series

  • Galaxy S21 Ultra (LTE/5G)
  • Galaxy S21+ (LTE/5G)
  • Galaxy S21 (LTE/5G)
  • Galaxy S20 Ultra (LTE/5G)
  • Galaxy S20+ (LTE/5G)
  • Galaxy S20 (LTE/5G)
  • Galaxy S20 FE (LTE/5G)
  • Galaxy S10 5G
  • Galaxy S10
  • Galaxy S10+
  • Galaxy S10e
  • Galaxy S10 Lite

Samsung Galaxy Note Series

  • Galaxy Note 20 Ultra (LTE/5G)
  • Galaxy Note 20 (LTE/5G)
  • Galaxy Note 10+ (LTE/5G)
  • Galaxy Note 10 (LTE/5G)
  • Galaxy Note 10 Lite

Samsung Galaxy Z Series

  • Galaxy Fold (LTE/5G)
  • Galaxy Z Fold 2 5G
  • Galaxy Z Flip
  • Galaxy Z Flip 5G
  • Galaxy Z Fold 3
  • Galaxy Z Flip 3

Samsung Galaxy A Series

  • Galaxy A71 5G
  • Galaxy A71
  • Galaxy A51 5G
  • Galaxy A51
  • Galaxy A52
  • Galaxy A52 5G
  • Galaxy A72
  • Galaxy A90 5G
  • Galaxy A01
  • Galaxy A11
  • Galaxy A31
  • Galaxy A41
  • Galaxy A21
  • Galaxy A21s
  • Galaxy A Quantum
  • Galaxy Quantum 2
  • Galaxy A42 5G
  • Galaxy A02
  • Galaxy A02s
  • Galaxy A12
  • Galaxy A32
  • Galaxy A32 5G
  • Galaxy A22 5G

Samsung Galaxy M Series

  • Galaxy M42 5G
  • Galaxy M12
  • Galaxy M62
  • Galaxy M02s
  • Galaxy M02
  • Galaxy M21
  • Galaxy M21s
    Galaxy M22
  • Galaxy M31
  • Galaxy M31 Prime Edition
  • Galaxy M51
  • Galaxy M31s

Samsung Galaxy F Series

  • Galaxy F41
  • Galaxy F62
  • Galaxy F02s
  • Galaxy F12
  • Galaxy F22

Samsung Galaxy Xcover Series

  • Galaxy Xcover Pro
  • Galaxy Xcover 5

Samsung Galaxy Tab Series

  • Galaxy Tab S7+ (LTE/5G)
  • Galaxy Tab S7 (LTE/5G)
  • Galaxy Tab S6 5G
  • Galaxy Tab S6
  • Galaxy Tab S6 Lite
  • Galaxy Tab A 8.4
  • Galaxy Tab A7
  • Galaxy Tab Active 3

Na hizo ndio baadhi ya simu ambazo zinategemewa kupata mfumo mpya wa One UI 4.0 (Android 12). Hata hivyo ni vyema kufahamu kuwa hii sio list yote kwani inawezekana kuongezeka pale kampuni ya Samsung itakapo tangaza rasmi list ya simu zote.

Kwa sasa kampuni ya Samsung imetengaza kuwa, inategemea kutoa sasisho jipya la One UI 3.5 kwa simu zote ambazo sasa zinatumia mfumo wa One UI 3.1.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use