Ni wazi kuwa smartphone bila apps ni sawa na “gari bila mafuta au bila umeme”, hii ni kwa sababu smartphone inaitwa “smart au janja” kutokana na uwezo wake wa kufanya kazi kwa kutumia apps mbalimbali na kurahisisha zaidi kazi ya mtumiaji.
Kuliona hili leo nataka nikupe urahisi zaidi wa kutumia simu yako hivyo nimekuletea apps hizi ambazo zinaweza kufanya simu yako kuwa janja zaidi pale unapo zitumia.
Najua huna muda mwingi wa kusoma maneno mengi hivyo moja kwa moja twende kwenye apps hizi ambazo na uhakika zitakusaidia kwa namna moja ama nyingine.
TABLE OF CONTENTS
CopyCat (Kuandika)
Kama wewe ni mmoja wa watu ambao hawataki kupoteza muda mwingi kuandika kitu chochote, iwe unataka kuandika email au barua pepe kwa kingereza, au unataka kuandika kitu chochote basi app hii itakusaidia sana.
App hii ina uwezo wa kuandika sentensi nzima au email nzima pale unapo andika kichwa cha habari pekee, yani kwa kuandika kichwa cha habari app hii itaweza kutengeneza email maalum kwaajili yako na utaweza kuitumia kwa kucopy na kuweka kwenye email yako. Jaribu app hii kisha nishukuru baadae.
Files Go (Mafaili)
Files Go ni app kutoka Google ambayo itakusaidia sana kuweza kuhakikisha simu yako inakaa kwenye hali ya usafi ikiwa pamoja na kuhakikisha simu yako haishiwi na nafasi. Uzuri wa programu hii ni kuwa inaweza kufanya yote hayo bila wewe kufanya chochote.
Unachotakiwa kufanya ni kuangalia ujumbe wa app hii kwenye sehemu ya Notification na utaona ukikwambia vitu kama vile unapokuwa na picha zinazo fanana, mafile makubwa au yanayo chukua nafasi kubwa pamoja na mapendekezo mengine mbalimbali ambayo yatasaidia sana kufanya simu yako kuwa safi kwa muda wote.
Picai (Kamera)
Picai ni app nyingine nzuri sana ambayo ni muhimu sana kwa wewe kuifahamu, app hii ni kwaajili ya kamera na itakusaidia kupiga picha zako kwa umakini kwa kutumia mfumo wa AI. Kupitia app hii utaweza kupiga picha kulingana na aina ya kitu.
Kupitia app hii nyooshea kamera yako kwenye kitu chochote unachotaka kupiga picha na moja kwa moja app hii itakujilisha kitu hicho ni nini na itakupa mapendekezo ya kutumia filter gani ili picha ya kitu icho itoke vizuri. App hii ni bora sana kama wewe ni mpenzi wa picha.
Truecaller (Simu)
Ni wazi kuwa simu zote ambazo ni smartphone zinakuja na sehemu ya kupiga simu, lakini ni wazi kuwa sehemu hiyo haina kila kitu ambacho pengine mtumiaji ungeweza kuhitaji. Kupitia app ya Truecaller utaweza kufanya mambo mengi sana kama nilivyoweza kueleza kwenye makala hapa.
Kuorodhesha baadhi ya mambo hayo ni pamoja na kupata ujumbe kabla mtu ajakupigia, kupata jina la mtu hata kama halipo kwenye simu yako, kutuma ujumbe wa tafadhali nipigie, kujua sababu ya mtu kukupigia simu kabla ya kupokea simu na mengine mengi.
Musixmatch (Muziki)
Ukweli ni kwamba kila mtu anapenda muziki, iwe ni mpenzi wa nyimbo za dini au nyimbo za kidunia ni wazi kuwa muziki ni sehemu ya muhimu kwenye maisha yetu. Japokuwa app ya Musixmatch sio app bora ya muziki lakini ni app bora sana pale unapo taka kujua mashairi ya nyimbo yoyote.
Kupitia app hii utaweza kupata mashairi ya nyimbo zote unazo sikiliza kupitia app hii, mbali na hayo ni kuwa mashairi hayo yanakuwa live au mubashara na nyimbo yenyewe pale inapo kuwa inaimba. Kizuri zaidi ni kuwa app hii inaweza kupata mashairi ya nyimbo za Kiswahili pia.
Curator (Picha)
Kama wewe ni mpenzi wa picha na umekuwa ukipiga picha nyingi kwenye simu yako kiasi cha kutojua picha fulani iko wapo basi, basi pengine app hii ya Curator ni muhimu kwako. Kupitia app hii utaweza kutafuta picha kulingana na picha yenyewe kwa urahisi kabisa.
Kama picha uliyopiga ilikuwa ni picha ya chakula basi unaweza kutafuta food kwenye app hii na itakuletea picha zote zenye chakula ambazo zipo ndani ya simu yako. Mbali ya hayo app hii inafanya yote hayo bila kutumia Internet na bure kabisa.
Hitimisho
Kwa sasa hizo ndio baadhi tu ya apps ambazo nimeona zinaweza kusaidia simu yako kuwa janja zaidi. Unaweza kudownload apps hizi kupitia link chini ya kila maelezo ya apps. Pia unaweza kutoa maoni yako unaonaje apps hizi au kama kuna app ambayo unataka tuongelee kupitia hapa basi pia unaweza kutuandikia kupitia sehemu ya maoni hapo chini.
Vinginevyo, kama unataka kujifunza zaidi kuhusu apps unaweza kusoma hapa kujua apps ambazo zitakusaidia kulinda afya yako kwa urahisi na haraka.