Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Microsoft Yazindua Mfumo Mpya wa Windows 11

Fahamu hapa yote ya muhimu kuhusu mfumo mpya wa Windows 11
Microsoft Yazindua Mfumo Mpya wa Windows 11 Microsoft Yazindua Mfumo Mpya wa Windows 11

Kampuni ya microsoft hapo siku ya jana ilizindua mfumo mpya wa Windows 11, mfumo ambao ni toleo la maboresho kwa Windows 10. Japo kuwa tumesha zoea kuwa Microsoft hufanya mabadiliko machache kwenye mifumo yake mpya, lakini hii ni tofauti kwa Windows 11.

Baada ya kufuatia uzinduzi wa mfumo huo hapo siku ya jana, yapo mambo mengi ambayo yalizungumziwa lakini yafuatayo ni mambo muhimu ambayo pengine ungependa kufahamu kuhusu mfumo huu mpya wa Windows 11.

Advertisement

Muonekano Mpya wa Windows 11

Kwa upande wa muonekano kampuni ya Microsoft imefanya mabadiliko makubwa huku mabadiliko hayo yakiwa yameangalia zaidi kwenye Menu mpya ambayo kwa sasa inapatikana katikati na unaweza kuchagua kuiweka popote unapotaka, tofauti na kwenye mfumo wa Windows 10.

Microsoft Yazindua Mfumo Mpya wa Windows 11

Mbali na hayo pia kupitia mfumo mpya wa Windows 11 utaweza kupata aina mpya kabisa ya rangi ambayo inakuja na muonekano ambao ni glass na pembe za duara kwenye kila programu utakayo fungua. Pia utaweza kupata sehemu mpya ya kugawa screen ya kompyuta yako kulingana na size ya kompyuta unayo tumia.

Microsoft Yazindua Mfumo Mpya wa Windows 11

Utaweza kutumia programu mbalimbali kwa pamoja kwenye kioo cha kompyuta yako, utaweza kuchagua mgawanyiko wa kioo kulingana na aina ya programu au kompyuta uliyo nayo.

Microsoft Yazindua Mfumo Mpya wa Windows 11

Mbali na hayo, pia Windows 11 inakuja na sehemu mpya ya Widgets ambazo unaweza kuzipata upande wa kushoto au wa kulia wa kompyuta hiyo. Kupitia sehemu ya Widgets unaweza kuweka shortcuts za vitu mbalimbali kama vile kalenda, saa, na vitu vingine kama hivyo.

Microsoft Yazindua Mfumo Mpya wa Windows 11

Windows 11 Kutumia Apps za Android

Mbali na mengine yote pengine jambo kubwa kuliko yote kuhusu mfumo mpya wa Windows 11 ni pamoja na uwezo wa mfumo huo kutumia apps za Android moja kwa moja kwa moja kwenye kompyuta.

Kwa mujibu wa Microsoft, watumiaji watakuwa na uwezo wa kuinstall apps za Android kwenye kompyuta moja kwa moja kupitia soko la Amazon Appstore. Watumiaji wa Windows 11 wanatakiwa kuwa na programu ya Amazon Appstore kwenye kompyuta ili kuweza kupakua apps ambazo zipo kwenye soko hilo moja kwa moja.

Kwa sasa bado haija julikana kama mtumiaji atakuwa na uwezo wa kuinstall apps kupitia apk au ni lazima kuwa na soko la Amazon Appstore ili kuweza kuinstall app hizo.

Microsoft Yazindua Mfumo Mpya wa Windows 11

Kama unataka kujua zaidi kuhusu sehemu hii endelea kutembelea Tanzania tech tutakujua jinsi ya kutumia sehemu hii ikiwa pamoja na kama sehemu hii inaweza kuwa na uwezo wa kupakia apk za apps za Android au ni lazima kuwa na soko la Amazon Appstore pekee.

Upatikanaji wa Windows 11

Kwa upande wa upatikanaji, Microsoft imetangaza kuwa mfumo wa Windows 11 unatagemewa kupatikana rasmi mwishoni mwa mwaka 2021, na watumiaji wa Windows 10 wataweza kupata mfumo huo bure kama update bila kununua.

Mahitaji ili Kupata Windows 11

Microsoft pia imeeleza sifa ambazo zinahitajika ili kompyuta yako iweze kutumia mfumo huo mpya wa Windows 11, sifa hizo ni pamoja na

  • Processor yenye gigahertz (GHz) 1 au zaidi, yenye core 2 au zaidi, ambayo pia ina uwezo wa 64-bit processor au System on a Chip au (SoC).
  • RAM GB 4 au zaidi.
  • SSD au HDD yenye nafasi ya hadi GB 64.
  • System firmware iwe ni UEFI, au Secure Boot capable.
  • Kompyuta yako iwe imewezeshwa na TPM au Trusted Platform Module (TPM) toleo la 2.0.
  • Graphics Card ya kompyuta yako iwe na uwezo wa DirectX 12 au WDDM 2.x.
  • Kioo cha kompyuta yako kiwe kuanzia inch 9 na kuendelea chenye resolution kuanzia 720p na kuendelea.
  • Pia kompyuta yako iwe na uwezo wa kuunganishwa kwenye Internet.

Angalia kama Kompyuta Yako itapata Windows 11

Mbali na hayo yote, kama unataka kuangalia kama kompyuta yako itakuwa na uwezo wa kufanyakazi vizuri ikiwa na mfumo wa Windows 11, unaweza kupakua programu hapo chini kutoka Microsoft kisha install na washa programu hiyo.

Download Programu Hiyo Hapa

Baada ya kufungua programu hiyo bofya sehemu ya Checknow kama inavyo onekana kwenye picha hapo chini.

Microsoft Yazindua Mfumo Mpya wa Windows 11

Baada ya muda mfupi utaweza kuona matokeo kama kompyuta yako inaweza kutumia mfumo wa Windows 11 au kama haiwezi pia utaweza kupewa ujumbe moja kwa moja.

Microsoft Yazindua Mfumo Mpya wa Windows 11

Kwa kufanya hatua hizo utakuwa upo tayari kupata mfumo mpya wa Windows 11 kwenye kompyuta yako, unacho takiwa kufanya ni kusubiri na utapata ujumbe moja kwa moja kuhusu update mpya ya Windows 11 bure kabisa bila kulipia kama unatumia mfumo wa Windows 10.

Na hayo ndio yote ya muhimu ambayo unatakiwa kufahamu kuhusu mfumo mpya wa Windows 11, kama unataka kujua zaidi unaweza kuangalia video hapo chini ambayo imeonyesha yote yaliyojiri kwenye uzinduzi wa mfumo huo hapo jana ndani ya dakika 7.

Kwa habari zaidi hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania tech kila siku, pia usisahau kujiunga na channel yetu kupitia mtandao wa YouTube ili kujifunza maujanja mbalimbali kwa vitendo, unaweza kubofya hapa kujiunga nasi leo.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use