Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Jinsi ya Kuhesabu Vitu Vingi kwa Kutumia Kamera ya Simu

Hesabu vitu zaidi ya milioni au zaidi ndani ya sekunde tano tu
Jinsi ya Kuhesabu Vitu Vingi kwa Kutumia Kamera ya Simu Jinsi ya Kuhesabu Vitu Vingi kwa Kutumia Kamera ya Simu

Kama wewe ni mmoja wa watu ambao mara nyingi hufanya kazi ya kuhesabu vitu mbalimbali basi pengine njia hii itaweza kukusaidia kurahisisha kazi kwa haraka.

Kupitia njia hii nitakuonyesha njia rahisi ambayo utaweza kutumia smartphone yako kuweza kuhesabu vitu mbalimbali kwa urahisi na haraka kwa kutumia kamera ya simu yako. Haijalishi kama una vitu milioni au zaidi kwa muda wa dakika moja utaweza kupata idadi ya vitu vyote kwa kutumia kamera ya simu yako.

Advertisement

Baada ya kusema hayo moja kwa moja twende kwenye hatua hizi rahisi ambazo najua zitaweza kukusaidia sana.

Kwa kuanza download app kupitia link hapo chini, baada ya kudownload moja kwa moja fungua app hiyo na kisha endelea kwenye hatua hapo chini.

Download App Hapa

Fungua app hiyo kisha tengeneza akaunti, kama huitaji kutengeneza akaunti basi moja kwa moja unaweza kubofya sehemu ya Continue as Guest.

Jinsi ya Kuhesabu Vitu Vingi kwa Kutumia Kamera ya Simu

Baada ya hapo bofya sehemu ya Got it kisha moja kwa moja utapelekwa kwenye ukurasa wenye template ambazo zitakusaidia kupata matokeo ya haraka, moja kwa moja chagua aina ya kitu ambacho unataka kuhesabu.

Unaweza kutumia sehemu ya kusearch iliyopo juu kabisa na kisha andika kitu unachotaka kuhesabu kwa mfano unaweza kuandika “Coins” kuhesabu pesa za coin kwa haraka.

Jinsi ya Kuhesabu Vitu Vingi kwa Kutumia Kamera ya Simu

Baada ya hapo moja kwa moja bofya sehemu ya Get kwenye matokeo, baada ya subiri kidogo na moja kwa moja utapelekwa kwenye ukurasa ambao unatakiwa kuchagua picha au kamera. Kama tayari unayo picha yenye coin nyingi au kitu chochote ambacho umechagua unaweza kuchagua picha hiyo kupitia sehemu ya Use Existing Photo iliyopo kushoto.

Lakini kama unataka kutumia kamera ya simu yako kuweza kuhesabu vitu hivyo moja kwa moja chagua sehemu ya Take New Photo ambayo ipo upande wa kulia.

Jinsi ya Kuhesabu Vitu Vingi kwa Kutumia Kamera ya Simu

Moja kwa moja baada ya kuchagua sehemu ya kamera app hii itafungua kamera ya simu yako na moja kwa moja elekeza kamera ya simu yako kwenye coin au kitu chochote ulicho chagua na kisha piga picha, hakikisha picha inakuwa na vitu vyote vikiwa ndani ya fremu.

Jinsi ya Kuhesabu Vitu Vingi kwa Kutumia Kamera ya Simu

Baada ya hapo subiria kidogo picha hiyo iweze ku-upload, na moja kwa moja baada ya sekunde chache utaweza kuona idadi ya coin au vitu ulivyoweza kupiga picha moja kwa moja kwa kutumia kamera ya simu yako.

Jinsi ya Kuhesabu Vitu Vingi kwa Kutumia Kamera ya Simu

Baada ya hapo unaweza kusave picha hiyo ikiwa na idadi ya vitu hivyo. Kama unataka kuhesabu kitu cha aina nyingine unaweza kuchagua templents mbalimbali kupitia sehemu ya Templates iliyopo chini kibiasa upande wa kulia.

Kwa kufuata njia hii natumaini utakuwa umepunguza kazi ya kuhesabu vitu vingi kwa kutumia muda mrefu. Kama unataka kujifunza zaidi hakikisha unasoma hapa kujua jinsi ya kutafsiti maandishi kwenda kwenye lugha yoyote kwa kutumia kamera ya simu yako. Kwa maujanja zaidi hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania tech kila siku.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use