Hivi karibuni kupitia hapa Tanzania tech tuliandika makala yenye kuhusu simu mpya ya Infinix ambayo inategemea kuja hivi karibuni ambayo pia itakuwa na chaja yenye teknolojia ya fast charging ya hadi 160W, lakini kama unakumbuka bado tulikuwa hatujui kuhusu jina la simu hiyo.
Sasa kwa mujibu wa habari mpya za hivi karibuni, Kampuni ya Infinix imetangaza rasmi kuwa ipo mbioni kuzindua simu mpya ya Infinix Zero X simu ambayo itakuwa ni simu ya kwanza ya aina hii kutoka Infinix. Mbali ya kuwa simu hiyo itakuwa inatumia chaja kubwa, simu hii pia itakuwa inatumia teknolojia ya wireless charging ambayo pia ina uwezo mkubwa wa hadi 50W.
Kupitia akaunti ya Twitter ya Infinix ya nchini India, kampuni hiyo ilipost kuhusu simu hiyo kama unavyoweza kuona tweet hapo chini.
Mbali na hayo, pia mvujishaji maarufu Ice Universe, hivi karibuni naye alipost kuhusu simu hiyo na kuweka picha hapo chini zinazo onyesha jina la simu hiyo ikiwa pamoja na chaja ya wireless yenye uwezo mkubwa wa 50W.
Kwa mujibu wa tovuti ya GSMArena, simu nyingi kwa sasa zinakuja na chaja za W100 na kuendelea, na simu chache zikiwa ziko mbioni kuja na chaja za 200W, hivyo simu hii ya infinix Zero X itakuwa ni moja kati ya simu ambazo zitakuwa kwenye kundi la simu zenye chaja za fast charging zenye uwezo mkubwa.
Hadi sasa bado hakuna tarehe halisi iliyotajwa na kampuni hiyo ambayo simu hiyo itazinduliwa rasmi, hivyo endelea kutembelea Tanzania tech kujua lini simu hii itazinduliwa ikiwa pamoja na kufahamu sifa zake pamoja na bei kwa hapa Tanzania.