Kampuni ya Infinix imekuwa maarufu kwa uzalishaji wa simu za bei nafuu, hivi karibuni kampuni hiyo imezindua simu mpya za Infinix Note 10 na Note 10 Pro. Lakini kama haitoshi sio siku nyingi sana kampuni hiyo pia imezindua toleo la bei nafuu la simu ya Infinix Hot 10, yaani infinix Hot 10t.
Lakini kwa mujibu wa habari mpya za hivi karibuni, kampuni ya Infinix iko mbioni kuja na simu mpya ambayo pengine ni tofauti na simu zote za Infinix ambazo zimewahi kutoka hadi sasa.
Kwa mujibu wa ripoti kutoka tovuti ya GSMArena, hivi karibuni zimevuja ripoti kuwa kampuni hiyo iko mbioni kuja na simu mpya ambayo itakuwa inatumia fast charging yenye uwezo wa 160W.
Mbali ya chaja hiyo, ambayo picha yale imevuja siku chache zilizopita, hivi leo imevuja picha nyingine kupitia mtandao wa XDA Developer, picha ambayo inasemekana kuwa ndio simu ambayo itakuwa inatumia chaja hiyo.
Kama unavyoweza kuona picha hapo juu, picha hiyo ndio simu mpya ambayo inatarajiwa kutumia chajia ya 160W ambapo bado hadi sasa haijajulikana simu hii itakuwa na battery ya ukubwa gani na wala bado jina la simu hii halijajulikana.
Kwa sasa kama inavyo onyesha kwenye picha, kuna neno “Now” nyuma ya simu hii kitu ambacho inasemekana kuwa neno hilo litakuwa sehemu ya msemo wa simu hiyo au sehemu ya jina la simu hiyo. Hadi sasa hakuna taarifa kamili wala tarehe ya uzinduzi wa simu hii kutoka kwa Infinix.
Kampuni ya Infinix hivi karibuni imejikita zaidi kwenye teknolojia mpya kwa kuingia rasmi kwenye biashara ya laptop, ambapo hivi karibu ilizindua laptop mpya ya Infinix InBook X1 na X1 Pro.
Hata hivyo kampuni hiyo kwa sasa inauza TV pamoja na Smartwatch huku pia ikimiliki mitandao mbalimbali ya kijamii ambayo inaendeshwa na kampuni ya Transsion Holdings ambayo ndio kampuni mama ya Infinix, Tecno pamoja na iTel.
Hadi tuna andika taarifa hizi bado hakuna taarifa kamili kuhusu simu hii mpya kutoka Infinix. Kama unataka taarifa zaidi endelea kutembelea Tanzania tech kila siku tutakuletea taarifa kamili.