Ni wazi kuwa wengi tunajua kuwa picha ikishapigwa ni ngumu sana kubadilika na kuwa video, lakini kupitia makala hii nitakuonyesha njia tofauti ambayo itakusaidia kubadilisha picha yoyote na kuwa video.
Kumbuka kuwa, hapa hatuongelei kuunganisha picha nyingi na kuzifanya ziwe video, hapana. Hapa tunaongelea kubadilisha picha moja ambayo imepigwa pekee na itaweza kubadilika na kuwa video.
Kwa mfano, kama umepiga picha yenye sura yako, kupitia njia hii utaweza kufanya sura kwenye picha hiyo kusogea kushoto na kulia, kutabasamu na mengine, yaani kama vile ulichukua video na sio picha. Unaweza kuona mfano hapo chini.
Kama unavyoweza kuona video hapo juu, kushoto ndio picha halisi, alafu kulia ndio video iliyo tengenezwa kutokana na picha hiyo.
Kama unataka kufanya picha zako ziwe video basi moja kwa moja twende kwenye makala hii, kwa kuanza unatakiwa kutembelea tovuti hapo chini.
Baada ya kuingia kwenye tovuti hiyo moja kwa moja bofya kitufe cha Upload Photo, hakikisha picha yako inayo sura na pia hakikisha picha yako inayo ukubwa wa angalau pixel 600 x 600. Hii itasaidia kupata matokeo mazuri zaidi ya video, pia hakikisha picha yako haina vitu vingi kwa nyuma.
Baada ya hapo moja kwa moja ukisha upload picha yako subiri kidogo na utaletewa fomu ya kutengeneza akaunti, hakikisha unatengeneza akaunti, kuharakisha unaweza kutumia mitandao ya kijamii kama vile Google, Facebook au unaweza kutumia barua pepe ili kutengeneza akaunti.
Baada ya hapo moja kwa moja utaweza kuona picha yako sasa ikibadilishwa na kuwa video na baada ya kumaliza utaweza kuona video yako ikicheza.
Baada ya picha kumaliza utaweza kuruhusiwa kudownload video yako kama utakuwa umerithika nayo, kumbuka unaweza kubadilisha picha kama umeona matokeo sio mazuri.
Baada ya hapo moja kwa moja utakuwa umeweza kubadilisha picha yako na kuwa katuni, kitu cha muhimu hakikisha picha yako inayo sura na hakikisha haina vitu vingi au rangi nyingi kwa nyuma. Picha ambazo zina rangi moja kwa nyuma huwa na uwezekano wa kuonekana vizuri zaidi kwenye video tofauti na picha zenye rangi tofauti kwa nyuma.
Kwa kufuata hatua hizo natumaini utakuwa umeweza kubadilisha picha yako kuwa video kwa urahisi kabisa. Kama unataka kujifunza zaidi hakikisha unasoma hapa jinsi ya kubadilisha video yoyote kuwa katuni kwa urahisi na haraka. Kwa maujanja zaidi endelea kutembelea Tanzania Tech.