Mtandao wa Spotify Wazinduliwa Rasmi Hapa Tanzania

Wasanii na wabunifu wa Tanzania wateza kuweka nyimbo na vipindi mbalimbali
Mtandao wa Spotify Wazinduliwa Rasmi Hapa Tanzania Mtandao wa Spotify Wazinduliwa Rasmi Hapa Tanzania

Mwaka jana 2020, kampuni ya Apple ilizindua rasmi mtandao wa Apple Music Hapa Tanzania, kwa sasa mtandao huo una nyimbo nyingi za wasanii kutoka hapa Tanzania na Afrika mashariki kwa ujumla.

Sasa baada ya kampuni ya Apple na mtandao wa Apple Music, hivi karibuni kampunia ya Spotify imetangaza kuzindua mtandao wake hapa Tanzania. Mtandao huo unaruhusu wasanii wa hapa nchini Tanzania kuweka nyimbo zao pamoja na vipindi vya mtandao kwa lugha yoyote ikiwa pamoja na Kiswahili.

Advertisement

Kwa ujumla mtandao huo utakuwa unapatikana kwa lugha mpya zaidi ya 36 ikiwa pamoja na lugha ya Kiswahili. Watumiaji wote wa hapa nchini Tanzania wataweza kujisajili na mtandao wa Spotify kwa kutengeneza akaunti ya bure na pia kulipia ili kuweza kusikiliza zaidi muziki na vipindi mbalimbali kutoka kwa wasanii na wabunifu mbalimbali.

Mbali ya Tanzania, Spotify inategemewa kuja kwenye nchini nyingine zaidi ya 80 ikiwa pamoja na nchi zote za Afrika mashariki pamoja na Afrika kwa ujumla. Kwa mujibu wa Cnet, list nzima ya nchi ambazo mtandao huo unategemewa kuzinduliwa hivi karibuni ni kama ifuatavyo.

  • Angola
  • Antigua and Barbuda
  • Armenia
  • Azerbaijan
  • Bahamas
  • Bangladesh
  • Barbados
  • Belize
  • Benin
  • Bhutan,
  • Botswana,
  • Brunei
  • Burkina Faso
  • Burundi
  • Cabo Verde
  • Cambodia
  • Cameroon
  • Chad
  • Comoros
  • Côte d’Ivoire
  • Curaçao
  • Djibouti
  • Dominica
  • Equatorial Guinea
  • Eswatini
  • Fiji
  • Gabon
  • Gambia
  • Georgia
  • Ghana
  • Grenada
  • Guinea
  • Guinea-Bissau
  • Guyana
  • Haiti
  • Jamaica
  • Kenya
  • Kiribati
  • Kyrgyzstan
  • Lao People’s Democratic Republic
  • Lesotho
  • Liberia
  • Macau
  • Madagascar
  • Malawi
  • Maldives
  • Mali
  • Marshall Islands
  • Mauritania
  • Mauritius
  • Micronesia
  • Mongolia
  • Mozambique
  • Namibia
  • Nauru
  • Nepal
  • Niger
  • Nigeria
  • Pakistan
  • Palau
  • Papua New Guinea
  • Rwanda
  • Samoa
  • San Marino
  • Sao Tome and Principe
  • Senegal
  • Seychelles
  • Sierra Leone
  • Solomon Islands
  • Sri Lanka
  • St. Kitts and Nevis
  • St. Lucia
  • St. Vincent and the Grenadines
  • Suriname
  • Tanzania
  • Timor-Leste
  • Togo
  • Tonga
  • Trinidad and Tobago
  • Tuvalu
  • Uganda
  • Uzbekistan
  • Vanuatu
  • Zambia and Zimbabwe

Spotify inatarajia kupataikana kwenye sehemu zote ikiwa pamoja na kwenye mtandao yaani website, apps zote za Android na iOS pamoja na apps za kwenye kompyuta. Pia inasemekana kuwa Spotify itaingia kwenye ushirikiano na kampuni mbalimbali kutangaza mtandao huo pamoja na kuweka app hiyo ndani ya vifaa mbalimbali kama smartphone, kompyuta na smartwatch.

Kwa sasa unaweza kupakua app ya Spotify kupitia link hapo chini, kisha jaribu kutengeneza akaunti ili kuanza kusikiliza kwa urahisi nyimbo za wasanii mbalimbali kutoka Afrika na dunia.

  • Android App

Download App Hapa

  • iOS App

Download App Hapa

Mtandao wa Spotify Wazinduliwa Rasmi Hapa Tanzania

Pia unaweza kutumia mtandao wa Spotify kwa lugha ya Kiswahili kupitia website yake kwa kutembelea mtandao huo kupitia link hapo chini.

Tembelea Tovuti Hapa

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use