Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Skip Matangazo ya YouTube Bila Kubofya Sehemu Yoyote

Utaweza kurusha matangazo YouTube bila kubofya sehemu ya Skip
Skip Matangazo ya YouTube Bila Kubofya Sehemu Yoyote Skip Matangazo ya YouTube Bila Kubofya Sehemu Yoyote

Kama wewe ni mtumiaji wa mtandao wa Youtube basi ni wazi kuwa kuna wakati unataka kuangalia video kupitia simu yako bila kubofya “Skip” ili kurusha tangazo. Mara nyingi hii inatokea kama umeshika simu yako kwa mkono mmoja.

Sasa kuliona hili leo nimekuletea njia rahisi ambayo unaweza kutumia ili kuweza “ku-skip” tangazo bila kubofya kwenye simu yako, njia hii inafanyakazi kwenye simu zote za Android na unaweza kurusha tangazo na kuendelea kuangalia video bila kubofya sehemu ya Skip.

Advertisement

Kumbuka njia hii haiondoi matangazo kwenye app ya YouTube bali inakusaidia kuweza kurusha matangazo ya video yanayotokea wakati una anza kuangalia video, katikati ya video au mwisho wa video.

Skip Matangazo ya YouTube Bila Kubofya Sehemu Yoyote

Kama unataka kurusha tangazo kwa urahisi bila kubofya sehemu ya Skip kwenye simu yako basi moja kwa moja twende kwenye hatua hizi.

Kwa kuanza, pakua app hapo chini. App hii ni bora lakini haipatikani kwenye soko la Play Store. Baada ya kupakua install kwenye simu yako kisha endelea kwenye hatua zifuatazo.

Download Hapa

Kwa kuanza baada ya kufungua app hii unatakiwa kuwasha app hii kupitia kwenye sehemu ya Accessibility, bofya sehemu ya Turn on na utapelekwa kwenye sehemu ya Accessibility kwenye simu yako.

Skip Matangazo ya YouTube Bila Kubofya Sehemu Yoyote

Baada ya kupelekwa kwenye sehemu ya Accessibility, shuka mpaka mwisho wa ukurasa kisha tafuta sehemu iliyo andikwa Ad Skipper.

Skip Matangazo ya YouTube Bila Kubofya Sehemu Yoyote

Utakuta sehemu hii ipo off, bofya hapo kisha bofya sehemu swichi iliyoko juu upande wa kulia kuweza kuwasha sehemu hii.

Skip Matangazo ya YouTube Bila Kubofya Sehemu Yoyote

Baada ya hapo rudi kwenye app hii kisha moja kwa moja utaweza kuona muonekano wa ambao utaonyesha sehemu ya kurusha matangazo imewezesha.

Skip Matangazo ya YouTube Bila Kubofya Sehemu Yoyote

Sasa moja kwa moja ingia kwenye app ya YouTube na fungua video yoyote yenye matangazo kisha subiri sekunde tano za kwanza zipite kwenye tangazo kisha utaona tangazo limeji rusha lenyewe. Kuthibitisha kama app hii inafanya kazi utaweza kurudi ndani ya app na utaweza kuona idadi ya matangazo yaliyorushwa na app hii tokea ulipo install app hii.

Skip Matangazo ya YouTube Bila Kubofya Sehemu Yoyote

Mbali na kurusha matangazo kwenye video, pia kupitia njia hii utaweza kuzima sauti ya matangazo hayo kabla ya kuyarusha, kama unataka kufanya hivyo unaweza kutumia sehemu ya Mute Ads inayo onekana kwenye ukurasa wa kwanza kwenye app hiyo kama inavyo onekana kwenye picha hapo chini.

Skip Matangazo ya YouTube Bila Kubofya Sehemu Yoyote

Kwa kufuata hatua zote hizo basi utakuwa umeweza kurusha au ku-skip ads kupitia app yako ya YouTube bila kubofya kitufe cha Skip. Kumbuka njia hii haiondoi matangazo kwenye app ya Youtube bali inakusaidia kurusha tangazo pale ambap una tumia mkono mmoja kuweza kuangalia video kwenye simu yako.

Kama unataka kujifunza zaidi unaweza kusoma hapa kujua njia bora ambayo itakusaidia kupakua video na audio kutoka kwenye mtandao wa YouTube kwa urahisi na haraka. Kwa maujanja zaidi hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania tech kila siku.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use