Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Mambo Uliyokuwa Hujui Kuhusu Mtandao wa YouTube

Haya ni baadhi ya mambo ambayo inawezekana ulikuwa hujui kuhusu Youtube
Mambo Uliyokuwa Hujui Kuhusu Mtandao wa YouTube Mambo Uliyokuwa Hujui Kuhusu Mtandao wa YouTube

Youtube ni moja kati ya mtandao mkubwa sana wa video, lakini pia youtube ni moja kati ya sehemu kubwa sana ya kutafuta vitu yaani kwa maneno mengine ni kuwa baada ya Google, Youtube ni sehemu nyingine ambayo hutumika zaidi kutafuta vitu mtandaoni.

Lakini leo hatuta angalia hayo bali natakanikujuze mambo haya muhimu ambayo kwa namna moja au nyingine ni muhimu wewe kujua, basi twende moja kwa moja….

Advertisement

  • Youtube Ilianzishwa Sababu ya Paypal

Mambo Uliyokuwa Hujui Kuhusu Mtandao wa YouTube

Mtandao wa Youtube uligunduliwa mwaka 2005 na Chad Hurley, Steve Chen, pamoja na Jawed Karim, watatu hawa walikuwa wanajuana kwa kuwa walikua wanafanya kazi sehemu moja yaani kwenye kampuni ya Paypal ambayo ni kampuni inayo jihusisha na mambo ya malipo kupitia mtandaoni. Hivyo kama sio watatu hawa kujuana kupitia kampuni hiyo labda leo mtandao wa Youtube usinge kuwepo.

  • Video ya Kwanza Kuwekwa kwenye Mtandao wa Youtube

Video ya kwanza kabisa kuwekwa kwenye mtandao wa youtube iliwekwa na mmoja wa watumiaji wa mwanzo wa mtandao huo Yakov Lapitsky, Video hiyo ilikuwa ikionyesha mmoja wa wagunduzi wa mtandao huo Jawed Karim akizungumzia kuhusu tembo video hiyo iliwekwa tarehe Apr 23, 2005. Unaweza kuangalia video hiyo hapo chini.

  • Mtandao wa Youtube Umezuiwa Kwenye Nchi Hizi

Mambo Uliyokuwa Hujui Kuhusu Mtandao wa YouTube

Kama wewe ni mmoja wa watuambao wanafaidi mtandao wa youtube kwa kujifunza mambo mbalimbali basi kumbuka kutumia vizuri mtandao huo kwani kwenye baadhi ya nchi serekali imekataza kutumika kwa mtandao huo kwa wakati mmoja au mwingine. baadhi ya nchi hizo ni pamoja na China, Iran, Syria, na Turkmenistan.

  • Video Ndefu Kuliko Zote Ina Muda wa Masaa 596.2

Video ambayo ina urefu kuliko video zote kwenye mtandao wa youtube ilikuwa na masaa 571, Dakika 1 na sekunde 41. Video hii ambayo sasa imeondolewa kwenye youtube ilikuwa inachukua muda wa siku 23 kuweza kuangalia video yote kupitia mtandao huo. Hadi sasa video ndefu kuliko zote ina muda wa masaa 596.2 na itakuchukua siku nzima kuweza kuangalia, video hii imewekwa kwenye mtandao wa YouTube mwaka 2011.

  • Mtoto Huyu Ndie anaetengeneza Pesa Zaidi YouTube (Kuliko watu wote)

Mambo Uliyokuwa Hujui Kuhusu Mtandao wa YouTube

Channel ya Ryan’s World ni channel iliyoanzishwa mwaka 2015 kipindi hicho channel hiyo ilikuwa inaitwa “Ryan ToysReview”. Channel hii ilianzishwa na Ryan Kaji, ambaye ni mtoto mwenye kati ya umri wa miaka 9 au 10 hadi mwezi wa sita mwaka 2020. Kwa sasa channel ya Ryan Kaji ambayo inaitwa “Ryan’s World” ndio channel inayo ingiza pesa nyingi zaidi kuliko channel nyingine zote kwenye mtandao wa YouTube.

Kwa mujibu wa Forbes, channel ya Ryan’s World kwa mwaka huu 2020 imetengeneza zaidi ya dollar za kimarekani milioni $29.5 ambayo hii ni sawa na takribani shilingi za kitanzania Bilioni 67.1 za kitanzania. Channel hii Ryan’s World sasa inayo zaidi ya subscriber milioni 47.7. Channel hii huonyesha video za mafunzo kwa watoto ikiwa pamoja na video za kisayansi kwa watoto.

  • YouTube Hutoa Bure Vifaa vya Kurekodia na Location Kupitia YouTube Space

Mambo Uliyokuwa Hujui Kuhusu Mtandao wa YouTube

YouTube Space ni sehemu maalum ambayo inamilikiwa na YouTube, sehemu hii imetengenezwa maalum kwaajili ya watu mbalimbali kwenda na kurekodi video zao bure kabisa ikiwa pamoja na kujifunza mambo mbalimbali. Kupitia kwenye majengo hayo ya YouTube Space, utaweza kupata kila kitu bure kama vile kamera za bure za kurekodia ikiwa pamoja na location mbalimbali zilizo tengenezwa maalum kwa ajili ya kurekodia.

Kitu cha muhimu unatakiwa kuwa na channel YouTube yenye zaidi ya Subscriber 10,000 ili kuruhusiwa kuingia kwenye majengo hayo ambayo yanapatikana nchi mbalimbali kama vile Berlin, London, Los Angeles, New York, Paris, Rio pamoja na Tokyo. Unaweza kufahamu zaidi kuhusu YouTube Space hapa.

Kwa sasa hayo ndio baadhi ya mambo ambayo huwenda ulikuwa hujui kuhusu mtandao wa YouTube. Kama unataka kujua zaidi unaweza kusoma hapa kujua mambo ambayo huwenda ulikuwa hujui kuhusu mtandao wa facebook.

5 comments
  1. Naomba kuulza,hv Channel za YouTube Zinatofautianaje?
    Zipo kwa ajiri ya business na ambazo sio,au zote ni kwa ajiri ya business?

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use