Ukweli ni kwamba logo ni kitu muhimu kwa biashara yoyote, iwe ni biashara ya mtandao au hata biashara yenye eneo maalum, logo ni moja ya utambulisho wa biashara yako.
Kwa sasa zipo njia mbalimbali za kulipa ambazo unaweza kutumia kutengeneza logo bora kwaajili ya biashara yako, lakini inakuwaje kama huna pesa za kulipia ili kutengenezewa logo kwaajili ya biashara yako.? Kuliona hilo leo nimekuletea njia bora na rahisi ya kutengeneza logo kupitia simu yako.
Njia hii ni rahisi na mtu yoyote mwenye simu ya Android anaweza kufanya hatua kwa hatua na hatimaye kuweza kutengeneza logo kwaajili ya biashara. Basi bila kupoteza muda zaidi twende moja kwa moja kwenye makala hii.
Kwa kuanza download app hapo chini kisha moja kwa moja endelea kwenye hatu zifuatazo, kumbuka unatakiwa kuwa na data kwenye simu yako.
Baada ya kudownload app hiyo na kuinstall kwenye simu yako, moja kwa moja bofya next iliyopo chini upande wa kulia.
Baada ya hapo Andika jina la biashara yako kisha bofya Next
Baada ya hapo moja kwa moja chagua category ya biashara yako, kama kwa namna yoyote hakuna category hiyo kwenye list basi chagua category ya business.
Baada ya hapo sasa upo tayari kuanza kutengeneza logo kwa kutumia simu yako, unaweza kuchagua logo mbalimbali kuingana na vikundi mbalimbali kama vile herufi na logo za kawaidia. Unaweza kuedit logo hizo kwa namna yoyote unayotaka na kusave kwenye simu yako moja kwa moja.
Unaweza kubadilisha kitu chochote kwenye logo hizi ikiwa pamoja na kuweka rangi au picha nyingine yoyote juu ya logo yako.
Unaweza kusave logo yako ikiwa kwenye format mbalimbali ikiwa pamoja na kuweka transparence kwenye logo yako kwa ajili ya kuweka kwenye vitu mbalimbali kama business card na vitu vingine.
Bila shaka kwa kufuata hatua hizo utakuwa umefanikiwa kutengeneza logo yako kwaajili ya biashara yako. Kumbuka unaweza kutumia app hii bila kulipia na utaweza kupata logo zaidi ya 1000 za kutumia kwenye biashara yako.
jina la app inaitwaje
naomba jina la hio app kwa sababu link hii haifunguki kwenye sim yangu
naomba mnitumie jila la hio app kwasababu kwangu siioni