Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Zifahamu Saa Mpya za Apple Watch Series 6 na Watch SE

Fahamu yote ya muhimu kuhusu saa mpya za Apple Watch Series 6 na Watch SE
Zifahamu Saa Mpya za Apple Watch Series 6 na Watch SE Zifahamu Saa Mpya za Apple Watch Series 6 na Watch SE

Mara baada ya kuangalia iPad Air (2020), hebu sasa twende moja kwa moja tukangalie saa mpya za Apple Watch Series 6 na Watch SE, zilizo zinduliwa hapo jana kwenye tamasha la Apple lililopewa jina la Time Files.

Apple Watch Series 6

Toleo jipya la Apple Watch Series 6 ni saa mpya ya Apple ambayo ni toleo la maboresho makubwa ya Apple Watch Series 5. Saa hii inakuja na chipset mpya ya S6, pamoja na processor ya dual-core ambayo Apple inadai ni inayo uwezo wa zaidi ya hadi asilimia 20%, kuliko toleo la Apple Watch S5.

Advertisement

Watch Series 6 imetengenezwa kwa chassis ya aluminum sawa na toleo lilopita la Watch Series 5, lakini mwaka huu Apple imeleta rangi mpya kwenye chassis hiyo ambapo sasa utaweza kupata Watch Series 6 yenye rangi ya Blue na Product Red kwenye chassis hiyo ya aluminum.

Zifahamu Saa Mpya za Apple Watch Series 6 na Watch SE

Chini ya saa hiyo mpya ya Apple Watch Series 6, kunayo sensor mpya ambayo inakuja na uwezo wa kupima kiwango cha kuenea kwa Oxygen kwenye damu maarufu kama Oxygen saturation (SpO2).

Zifahamu Saa Mpya za Apple Watch Series 6 na Watch SE

Mbali na hayo, sasa kupitia saa hiyo pamoja na mfumo mpya wa WatchOS 7, utaweza kufuatilia mpangilio wa usingizi au kulala, ikiwa pamoja na mfumo mpya wa kukusaidia kunawa mikono vizuri, moja kwa moja na aina mpya za mazoezi.

Zifahamu Saa Mpya za Apple Watch Series 6 na Watch SE

Apple Watch Series 6 pia inakuja na maboresho kwenye mpangilio wa Always-On display mode, ambapo sasa kioo cha saa hiyo kinakuja na uwezo wa mng’ao brightness mara mbili na nusu zaidi ya mpangilio huo kwenye toleo la zamani la saa ya Apple Watch Series 5.

Mbali na hayo saa hiyo mpya pia inakuja na aina mpya 7 za nyuso za saa hiyo, ikiwa pamoja na Stripes, Chronograph Pro, GMT, pamoja na Artist.

Zifahamu Saa Mpya za Apple Watch Series 6 na Watch SE

Apple pia imezindua mikanda mipya ya saa hizo za Watch Series 6, ambayo inakuja ikiwa haina sehemu ya kufungia, bali mikanda hiyo itakuwa ni ya moja kwa moja na inaweza kutanuka kumtosha mtu yoyote wakati wa kuvaa, na pia inapatikana kwa size mbalimbali.

Kwa upande wa Battery, Apple Watch Series 6 inasemekana kuja na battery inayo lingana na Watch Series 5, huku saa hiyo ikiwa na maboresho ya teknolojia ya Fast charging ambayo inasaidia kuchaji kwa haraka saa hiyo ya Watch Series 6 hadi kujaa kwa muda wa lisaa limoja tu.

Bei ya Apple Watch Series 6

Kwa upande wa bei, saa ya Apple Watch Series 6 inategemewa kuanza kupatikana kuanzia September 18, huku Watch Series 6 yenye uwezo wa GPS pekee itauzwa kwa dollar $399 ambayo ni sawa takribani TZS 926,000 bila kodi kwa saa yenye size ya 40mm.

Watch Series 6 yenye GPS na size ya 44mm itauzwa kwa dollar $429, ambayo ni sawa na takribani TZS 996,000 bila kodi.

Saa hiyo yenye uwezo wa GPS pamoja na uwezo wa simu (Cellular) itapatikana kwa dollar $499 au $529 ambayo ni sawa na takribani TZS 1,158,000 au TZS 1,228,000 kulingana na ukubwa. Kumbuka bei zote hizi ni bila kodi, pia kumbuka bei hizi zinaweza kubadilika kulingana na sehemu utakayo nunua pamoja na kodi. Kufahamu zaidi kuhusu Watch Series 6 Soma hapa.

Apple Watch SE

Kwa upande wa Watch SE, kampuni ya apple ilizindua saa hiyo ambayo itakuwa ya bei nafuu zaidi huku ikiwa na baadhi ya sifa za Watch Series 5 ambayo ni pamoja na chipset yake, muundo, pamoja na sensor ya kupima mapigo ya moyo.

Mbali na hayo, Watch SE inakuja na sensor za accelerometer, gyroscope na always on altimeter ambazo zinafanana na zile zilizopo kwenye saa mpya ya Watch Series 6.

Zifahamu Saa Mpya za Apple Watch Series 6 na Watch SE

Apple Watch SE inakuja na baadhi ya sifa zinazofanana lakini pia inakuja na mfumo wa kugundua pale mtu aliye ivaa anapo anguka. Mbali ya hayo saa hii inakuja na sifa zinazofanana na Series 5.

Zifahamu Saa Mpya za Apple Watch Series 6 na Watch SE

Bei ya Apple Watch SE

Apple Watch SE yenye 40mm inapatikana kwa dollar za marekani $279 ambayo ni sawa na taribani TZS 648,000 bila kodi. Saa hiyo yenye ukubwa wa 44mm itapatikana kwa dollar $309 ambayo ni sawa na takribani TZS 717,000 bila kodi. Saa hiyo yenye uwezo wa kupiga simu inapatikana kwa dollar $329 au $359 ambayo ni sawa na takribani TZS 764,000 au 833,000 kulingana na ukubwa.

Kumbuka bei zote ni bila kodi, pia kumbuka bei hizi zinaweza kubadilika kulingana na sehemu utakayo nunua, viwango vya kubadilisha fedha pamoja na kodi. Kufahamu zaidi kuhusu Watch SE soma hapa.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use