Moja kati ya programu moja ya muhimu ya kuedit video ni programu ya KineMaster, programu hii inaweza kukusaidia sana kuedit video kwa urahis na haraka kwenye simu yako na moja kwa moja kushare video hiyo kwenye mitandao ya kijamii kama YouTube, Facebook, Instagram na mitandao mingine mbalimbali.
Programu ya KineMaster inapatikana kupitia kwenye soko la Play Store bure kabisa, lakini programu hii inakuja na alama ambazo zinakuwa kwenye video zako pale utakapo share video zako kwenye mitandao ya kijamii, kuondoa alama hiyo ni lazima kulipia ili kuweza kuondoa alama hiyo.
Kuliona hilo leo Tanzania tech tunaletea njia mpya na rahisi ya kuweza kupata programu ya KineMaster Pro kwa ajili ya majaribio bure bila kulipia. Programu hii inakuja na sehemu nyingi sana ambazo zinaweza kukusaidia kushare video angavu na zenye muonekano mzuri sana.
Zifuatazo ni baadhi ya sifa za programu ya KineMaster Pro, kumbuka toleo la Pro ni toleo la kulipia na utaweza kulipata bure kwa majaribio kupitia njia hii.
- Kupitia KineMaster Pro, unaweza kuchanganya safu nyingi za video, picha, stika,
- Unaweza kurekebisha rangi pamoja na kupata zana za kurekebisha rangi.
- Programu hii pia inaweza kutumika kugeuza picha za kawaida kuwa video.
- Pia kupitia programu unaweza kuchanganya video pamoja na Sound Effect mbalimbali.
- Unaweza pia kuweka sauti kwenye video, muziki, sound effect na vitu vingine mbalimbali
- KineMaster Pro, pia inakupa uweza kuwa kuongeza au kupunguza kasi ya video kwa urahisi na haraka.
- Pia unaweza kuweka maandishi kwenye video zako kwa haraka huku ukiwa na uwezo wa kubadilisha font au muandiko.
- Na pia, unaweza kushiriki video zilizo haririwa moja kwa moja kwenye tovuti za mitandao ya kijamii.
- Na mambo mengine mengi
Kumbuka Programu hii ni kwa ajili ya majaribio, kama unataka kupata programu hii unaweza kununua kupitia kwenye soko la Play Store. Kama unataka kujifunza zaidi unaweza kusoma hapa kujua jinsi ya kuangalia Movie kwenye mtandao wa Neflix bure na bila kulipia wala kuwa na akaunti.
Kwa maujanja zaidi kwa vitendo hakikisha una jiunga na channel yetu ya Tanzania Tech kupitia mtandao wa YouTube hapa. Kwa habari za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech kila siku.