Wakati corona ikiwa imeathiri kampuni nyingi za teknolojia, lakini bado kampuni hizo zimeonekana kuendelea na ratiba yake ya kuzindua simu zake. Mfano wa kampuni hizo ni kampuni ya TECNO ambayo hivi karibuni ilizindua simu mpya za TECNO Spark 5.
Lakini kama bado haitoshi, kampuni hiyo imeendelea na ratiba yake ya kawaida kwa kutarajiwa kuzindua simu mpya ya TECNO Phantom 10 ambayo inatarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni.
Japo kuwa bado hakuna uhakika kama simu hiyo itakuwa na jina la Phantom 10, lakini ni wazi kuwa simu hiyo ni toleo la Phantom ambalo huzinduliwa na TECNO kila mwaka.
Kwa sasa tetesi za ujio wa simu hiyo bado zinaendelea kusambaa huku baadhi ya vyanzo vikitaja sifa mbalimbali za simu hiyo. Kwa mujibu wa vyanzo hivyo, inasemekana Phantom 10 itakuja na uhifadhi wa ndani wa GB 128, RAM ya GB 8 pamoja na CPU ya octa-core Mediatek Helio G70 ambayo imetengenezwa maalum kwa ajili ya game.
Mbali na hayo inasemekana kuwa simu hiyo itakuja na kioo kikubwa cha inch 6.8 huku kikiwa kimetengenezwa kwa teknolojia ya AMOLED Display.
Hata hivyo inasemekana simu hizo zitakuja kwa matoleo mawili, toleo la TECNO Phantom 10, pamoja na toleo la TECNO Phantom 10 Premier. Kwa sasa bado hatuja jua simu hizo zina tofauti gani lakini pengine tegemea kuona uwezo tofauti wa kamera na battery kwenye kila simu.
Tukiongelea upande wa battery, inasemekana kuwa simu hizi zitakuja kwa matoleo mawili toleo la kwanza likiwa na battery kubwa ya mAh 5000 na toleo lingine likiwa na battery ya mAh 4000.
Pia inasemekana kuwa simu hizo zote zitakuja na mfumo mpya wa Android 10, huku kwa mara ya kwanza simu hiyo ikiwa na aina mpya ya USB Type C ambayo hapo kwenye simu nyingi za TECNO hata za daraja la juu.
Kwa sasa bado hatuja fahamu tarehe halisi ya uzinduzi wa simu hiyo, hivyo endelea kutembelea Tanzania Tech tutakufahamisha pindi tutakapo pata habari zaidi.