Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Programu za Kusaidia Kutafuta Mafile kwenye Kompyuta (Windows)

Programu hizi ni kama tovuti ya Google lakini hii ni kwaajili ya kompyuta yako
Programu za Kusaidia Kutafuta Mafile kwenye Kompyuta (Windows) Programu za Kusaidia Kutafuta Mafile kwenye Kompyuta (Windows)

Kama wewe ni mtumiaji wa kompyuta yenye mfumo wa Windows basi karibu kwenye makala nyingine ambayo na uhakika itakwenda kukusaidia kuboresha matumizi ya kompyuta kwa kiasi kikubwa.

Kupitia makala hii itaenda kuonyesha programu za Windows ambazo zitakusaidia sana kuweza kutafuta vitu kwa haraka kwenye kompyuta yako. Kama wewe ni kama mimi una vitu vingi kwenye kompyuta yako basi hakika programu hizi zitakufaa sana.

Advertisement

Programu za Kusaidia Kutafuta Mafile kwenye Kompyuta (Windows)

Kama unavyoweza kuona hapo juu ni picha ya kompyuta yangu ambayo mara nyingi natumia kwa kazi mbalimbali, unaweza kuona hapa utafutaji wa baadhi ya vitu lazima unakuwa mgumu sana kutokana na kuwepo kwa vitu vingi sana kwenye kompyuta.

Hapo mwanzo nilikua natumia sehemu ya kutafuta ya Windows ambayo ipo upande wa kushoto chini, lakini sehemu hiyo haiwezi kukusaidia kwa kiasi kikubwa hasa kama kompyuta yako imeunganishwa na internet.

Hiyo ni kwa sababu sehemu hiyo hutoa matokeo ya mtandaoni hivyo kushindwa kusaidia kutafuta vitu vilivyopo ndani ya kompyuta yako au ndani ya mafile yaliyopo kwenye kompyuta yako.

Lakini kupitia makala hii nita share na wewe programu ambazo ni kama Google ya kompyuta yako kwani zinaweza kusaidia kutafuta mafile yote yaliyo ndani ya kompyuta yako. Basi bila kupoteza muda twende tuangalie programu hizi.

Wise JetSearch

Programu za Kusaidia Kutafuta Mafile kwenye Kompyuta (Windows)

Wise JetSearch ni programu nzuri sana ambayo inakusaidia kusearch mafile kwenye kompyuta yako. Uzuri wa programu hii inauwezo wa kutafuta mafile kwenye sehemu mbalimbali ikiwa pamoja na kwenye flash au hard disk ambazo utakuwa umechomeka kwenye kompyuta yako. Programu hii ni bure kabisa kutumia na inauwezo mkubwa sana.

Download Wise JetSearch

Everything

Programu za Kusaidia Kutafuta Mafile kwenye Kompyuta (Windows)

Everything ni programu nyingine ambayo itakusaidia kusearch mafile kwa haraka kwenye kompyuta yako. Uzuri wa programu hii ni rahisi kutumia na inao uwezo mkubwa sana wa kutafuta mafile ya aina mbalimbali. Programu hii ni nyepesi sana na inaweza kufanya kazi hata kwenye kompyuta za zamani za Windows au kompyuta zenye uwezo mdogo.

Download Everything

Quick Search

Programu za Kusaidia Kutafuta Mafile kwenye Kompyuta (Windows)

Quick Search ni programu nyingine ambayo itakusaidia kupata mafile yako kwa haraka zaidi, programu hii kama zilivyo programu zilizo tangulia, inao uwezo mkubwa wa kutafuta mafile yote kwa haraka na pia ni rahisi sana kutumia. Unacho takiwa kufanya ni kutafuta mafile kwakuandika na moja kwa moja utaweza kupata kwa haraka unachotafuta.

Download Quick Search

Duplicate File Finder

Programu za Kusaidia Kutafuta Mafile kwenye Kompyuta (Windows)

Tofauti na programu nyingine kwenye list hii, programu ya Duplicate File Finder ni programu itakayo kusaidia kutafuta mafile yaliyo jirudia kwa haraka na urahisi. Kama unayo mafile mengi kwenye kompyuta yako na unahisi kuwa inawezekana kuwa kuna mafile yaliyo jirudia basi programu hii ni muhimu kwako. Kupitia programu hii utaweza kutafuta mafile yote kwa haraka na kuweza kufuta mafile hayo yaliyo jirudia kwa urahisi na haraka.

Download Duplicate File Finder

SearchMyFiles

Programu za Kusaidia Kutafuta Mafile kwenye Kompyuta (Windows)

SearchMyFiles ni programu nyingine ya kutafuta mafaili, programu hii ni nzuri lakini inafaa zaidi kwa wale wenye ujuzi kidogo wa kompyuta. Programu hii inaweza kufauta mafaili ya aina yoyote lakini kama unavyoweza kuona hapo juu programu hii inakua na sehemu nyingi za kuchagua hivyo inaweza ikawa ngumu kidogo kutumia. Lakini mbali ya hayo programu hii ni nzuri sana.

Download SearchMyFiles

UltraSearch

Programu za Kusaidia Kutafuta Mafile kwenye Kompyuta (Windows)

Programu ya mwisho kwenye list hii ni programu ya UltraSearch, programu hii ni nzuri sana na inaweza kukusaidia sana kutafuta mafile mbalimbali. Programu hii ni nzuri lakini inao uwezo wa kutafuta mafile yaliyo ndani ya kompyuta yako tu na hutoweza kutafuta mafile yaliyopo kwenye flash au Hard Disk.

Na hizo ndio programu bora ambazo zinaweza kukusaidia kutafuta mafile kutoka kwenye kompyuta yako, kama unataka kujifunza zaidi kwa vitendo nakusihi ungana nasi kupitia channel yetu ya mtandao wa YouTube hapa.

Kwa makala zaidi soma hapa kujua programu ambazo zinaweza kukusaidia kudownload kwa haraka kwenye kompyuta yako ya Windows. Kujifunza zaidi hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania Tech kila siku.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use